loader
Picha

Shibuda ataka JPM amulike watendaji wanaokwamisha mikutano yao

MWENYEKITI wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, John Shibuda amemwomba Rais John Magufuli kumulika baadhi ya watendaji wake hususan wenye mamlaka na masuala ya siasa kwa madai wamekuwa kikwazo na kusababisha masuala ya kujadiliana ndani ya nchi kwenda kuzungumzwa nje ya nchi.

Shibuda amesema sehemu ya siha kwa wadau kuzungumzia masuala ya siasa nchini ni kupitia vikao vya ndani ya baraza hilo na kwenye mafunzo lakini hayo hayafanywi na hakuna sababu zinazotolewa.

Amesema mara ya mwisho walikutana mwaka jana kabla ya  Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na baada ya hapo, vikao vya kamati ya uongozi vilifuatia lakini hadi leo hakuna kikao kingine cha baraza hilo.

Hata hivyo, akizungumzia hoja ya Shibuda, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji mstaafu Francis Mutungi amesema serikali imetoa fedha kwa ajili ya baraza hilo na mambo mengine na kwamba muda muafaka utakapofika kikao cha baraza hilo kitaitishwa.

BUNGE limeelezwa kuwa kipindi cha pili cha Mpango wa Kunusuru ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi