loader
Picha

Wanafunzi wawezeshwa kusoma kidijitali

KATIKA jitihada za kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19, unaosababishwa na virusi vya corona, Kampuni ya Vodacom Tanzania imewawezesha wanafunzi ambao kwa sasa wamefunga shule, kupata nyenzo za kujisomea kwa njia ya kidijitali.

Aidha kampuni hiyo inatoa fursa ya kupata taarifa za corona bila malipo kupitia katika tovuti mbalimbali za serikali, zikiwemo tovuti za Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Idara ya Habari (Maelezo).

Akizungumza Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Hisham Hendi amesema, “Wakati huo tunaweka juhudi za pamoja na watanzania kwa kuwasaidia wanafunzi waliofunga shule ili waweze kupata nyenzo za kujisomea kwa njia ya kidijiti kwa kutumia mitaala inayokubalika kimataifa.

Kupitia mfumo uliopitishwa kimataifa wa Khan Academy http://instantschools.vodacom.co.tz/user/#/sign in, wanafunzi ambao wako nyumbani kutokana na janga hili, wanaweza kuendelea kujisomea, na kuchukua hatua stahiki za kujikinga na ugonjwa wa covid-19.

Pia, Mkurugenzi huyo alisema watumiaji wa Vodacom na wasiokuwa watumiaji, wanaweza kupata huduma ya Shule Papo Hapo (Vodacom Instant Schools) bila malipo yoyote.

Alieleza kuwa jukwaa hilo ni huru kwa wote, ambapo watumiaji wa Vodacom wanaweza kupata masomo mbalimbali kwa kuzingatia mitaala ya shule za msingi na sekondari, yanayohusisha majaribio, chemsha bongo na video za masomo.

Katika kuimarisha usalama wa wafanyakazi wake, Hendi alisema zaidi ya wafanyakazi wake 560 wanafanya kazi kutoka majumbani kwa kiwango cha juu huku wakitoa huduma bora kwa zaidi ya wateja wao zaidi ya milioni 14, kwa kuzingatia miongozo ya serikali na wizara zake.

“Mafanikio katika kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu yatategemea nguvu ya pamoja kutoka kwa kila raia katika kuchukua jukumu la kuzuia kuenea kwa janga hili,” amesema.

Aliongeza kuwa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, wanatoa huduma ya ujumbe mfupi (SMS) kwa wateja nchi nzima juu ya usafi na taarifa nyingine zinazohusu ugonjwa huo.

JAJI Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania, Dk Eliezer Feleshi amewataka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi