loader
Picha

Maambukizi corona duniani bado yako juu

HALI ya maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha homa ya mapafu bado iko juu, Chuo Kikuu cha Johns Hopkins kimesema.

Chuo hicho kimesema, katika nchi za China, Italia, Marekani, Hispania, Ujerumani, Iran, Ufaransa, Uswisi, Uingereza, Korea Kusini, Netherlands na Austria zinaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi kuanzia wagonjwa 5,000. Imeelezwa, Afrika Kusini inaongoza Afrika kwa kuwa na wagonjwa wengi wa corona.

Chuo kimesema China kwa sasa ina wagonjwa 81,667 wa corona na vifo 3,285, ikifuatiawa na Italia yenye wagonjwa 74,386 na vifo 7,503.

Nyingine ni Marekani yenye wagonjwa 68,795 na vifo 1,037, Hispania wagonjwa 49,515 na vifo 3,647, Ujerumani wagonjwa 37,323 na vifo 206, Iran wagonjwa 27,017 na vifo 2,077. Nchi nyingine zenye maambukizi ya juu ni Ufaransa yenye wagonjwa 25,233 na vifo 1,331, Uswisi wagonjwa 10,897 na vifo 153.

Nchi nyingine ni Uingereza yenye wagonjwa 9,529 na vifo 465, Korea Kusini wagonjwa 9,137 na vifo 126, Uholanzi wagonjwa 6,412 na vifo 356 na Austria wagonjwa 5,588 na vifo 30.

Barani Afrika, Afrika Kusini ndiyo yenye wagonjwa wengi, 709 na hakuna kifo. Takwimu za tovuti ya ‘worldometers’ zinaonesha duniani kuna wagonjwa 471,794 na vifo 21,297, waliotibiwa na kupona 114,703.

Kutokana na kuenea kwa maambukizi hayo, nchi mbalimbali duniani zimechukua hatua madhubuti za kukabilianana virusi hivyo.

Hatua hizo ni pamoja na kuweka karantini nchi nzima, kufunga mipaka, watu kukaa karantini siku 14, kupulizia dawa maeneo mbalimbali na kutoa elimu ya kwa wananchi kujikinga corona.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Arumeru imewafutia mashitaka washitakiwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi