loader
Picha

Anayedaiwa kuua ‘hausigeli’ kizimbani tena

MWANAMKE mkazi wa Arusha, Mkami Shirima (30) anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya mfanyakazi wa ndani, Salome Zakaria (18) leo amefikishwa tena Mahakama ya Wilaya ya Arumeru Sekei, Arusha.

Mkami alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Amalia Mushi kwa mara ya pili huku akiwa amejifunika sura yake kwa mtandio.

Wakili wa Serikali, Abelaide Kasala aliiambia mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Mushi alikubaliana na hoja hiyo na kuahirisha kesi hadi Aprili 8, mwaka huu itakapotajwa tena.

Awali Machi 14, mwaka huu mshitakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza na kusomewa shitaka la mauaji ambalo mshitakiwa anadaiwa kumuua Salome Zakaria, Machi 6, mwaka huu.

Mshitakiwa huyo baada ya kuahirishwa kesi hiyo, alipandishwa kizimbani tena mbele ya Hakimu Gwantwa Mwankuga kwa kesi nyingine ya kusafirisha dawa za kulevya (mirungi) kilogramu 2.9.

Mbele ya Hakimu Mushi, Wakili wa Serikali, Naomi Mollel ameomba mahakama hiyo itoe hati ya kuongeza muda wa upelelezi wakati wakisubiri ripoti kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Hakimu Gwantwa ameahirisha kesi hadi Aprili 8, mwaka huu na watuhumiwa wakaachiwa kwa dhamana.

Mshitakiwa huyo na mwenzake, Emiliana Laizer walifikishwa hapo mara ya kwanza Novemba 11, 2019.

Ilidaiwa Septemba 24, 2019 eneo la Mianzini bila uhalali walikutwa wakisafirisha mirungi kilo 2.9.

BUNGE limeelezwa kuwa kipindi cha pili cha Mpango wa Kunusuru ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Arusha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi