loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Idris Elba amzodoa Cardi B

MWIGIZAJI na mwanamuziki Idrissa Elba amewapasha wale wanaosema kuwa watu mashuhuri wanalipwa kwa kusema wana virusi vya corona.

Elba wiki iliyopita alipimwa na kukutwa na virusi vya ugonjwa wa Covid-19, na amesikitika watu matajiri wanaonekana wanapima zaidi kuliko maskini na kupinga kauli za watu kusema watu mashuhuri wamepewa pesa kusema wana virusi.

Mmoja wa watu waliosema mastaa wanalipwa kusema wana virusi vya corona ni msanii Belcalis Marlenis Almánzar ‘Cardi B’ na kuhoji ilikuwaje wakaenda kupima wakati hawana dalili zozote?

Kupitia InstaLive Elba alisema: “Wazo hili mtu kama mimi naweza kulipwa kusema nina ugonjwa, ni jambo ambalo halina maana, huu ni ujinga na watu wanataka kueneza utadhani kama ni habari na njia ya haraka ya kuwafanya watu wapate maambukizi”

Aliongezea: “Mimi ni binadamu na kioo cha jamii. Kwa hivyo nataka watu waelewe kuwa ni kweli nilipata mtihani huu,” Hapo awali Elba alielezea alipimwa virusi, licha ya kuwa hakuwa na dalili baada ya kuwasiliana na mtu ambaye alikuwa na kipimo. Jana Elba aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa: “Natumaini kila mtu anapambana na janga hili.

Bado niko kwenye karantini, ninajiona bado, hakuna mabadiliko. Daktari alituambia baada ya kutuweka karantini kinga zetu zitapambana, kweli zilipambana na virusi hivi. Wakati mwingine tunapenda kwenda nyumbani London.

Muwe salama,” Elba mwenye umri wa miaka 47 na mkwe Sabrina Dhowre-Elba wote wanaugua virusi vya corona na wapo kwenye karantini.

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, amewataka mashabiki wa timu hiyo ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi