loader
Picha

Ndalichako aahidi kuisadia shule inayojengwa na Bunge

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewaagiza watendaji wake kuanza ukaguzi wa shule ya wasichana inayojengwa na bunge ili kutoa ushauri ambao utasaidia usajili kufanyika kwa wakati.

Pia ameahidi kuunga mkono juhudi za wabunge katika ujenzi wa shule hiyo inayojengwa katika Kata ya Kikombo Jiji la Dodoma.

Ndalichako ametoa kauli hiyo jijini hapa baada ya kualikwa na Spika, Job Ndugai ili kujionea maendeleo ya ujenzi huo.

Aidha, Profesa Ndalichako amewaagiza Kamishna wa Elimu, Dk Lyabwene Mtahabwa na Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora wa Shule, Euphrasia Buchuma kuanza hatua za ukaguzi wa shule hiyo ili usajili ufanyike kwa wakati pindi itakapokuwa imekamilika.

BUNGE limeelezwa kuwa kipindi cha pili cha Mpango wa Kunusuru ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi