loader
Picha

Wanaofanya biashara maeneo yasiyo rasmi waonywa

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imewataka wafanyabishara wanaofanya biashara zao kwenye maeneo yasiyo rasmi ikiwemo kwenye barabara kuondoka kwa kuwa ni maeneo hatari kiusalama na kiafya.

Ofisa Masoko wa jiji hilo, James Yuna aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wa wafanyabiashara hao kuhusiana na kampeni endelevu ya kuwaondoa wale wote wanaopanga biashara zao katika maeneo yasiyo rasmi.

Alisema maeneo kama barabara za magari na watembea kwa miguu, darajani, mitaroni ni hatari kwao na wateja huku akiwataka kufanya biashara kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya biashara hizo badala ya kuvamia kufanya biashara maeneo yasiyo rasmi kwao.

Aliwataka viongozi kushirikiana na jiji kutoa elimu ili kuondoa tatizo la kufanya biashara bila mpangilio wowote.

“Wengi wao wamepanga biashara kwenye maeneo yasiyo rasmi kama vile katika mitaro ya maji, kwenye madaraja na barabarani, ninachowaambia hatutakubali kuona sheria na kanuni zinapuuzwa hivyo ni vyema mkajiondoa wenyewe,”alisema.

Yuna pia aliwataka wafanyabiashara kufanya biashara kwenye masoko yaliyopo karibu kwenye kata zote kwa kuwa nafasi bado zinapatikana. Naye, Katibu wa wafanyabiashara hao, Victor Sijila aliwataka wenzake kutambua kuwa mtu kuwa na vitambulisho vya machinga isiwe sababu ya kukiuka sheria na kanuni zilizowekwa na halmashauri kwa kufanya biashara holela bila mpangilio.

Alisema wao kama viongozi wanaunga mkono oparesheni ya kuwaondoa wale wote wanaokiuka sheria na kanuni kwa kufanya biashara kwenye maeneo yasiyo rasmi.

Katibu huyo alisema kuwa baadhi ya wafanyabiashara ho wamepanga bidhaa zao kwenye maeneo hatarishi na hakuna sababu ya kukaidi kuondolewa kwenye maeneo hayo ambayo si rasmi kwao kufanyia biashara.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa maagizo ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi