loader
Picha

Mvua yavuruga eneo la mwekezaji, kupewa lingine

KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na serikali mkoani hapa wameahidi kumtafutia eneo mbadala mwekezaji wa kilimo cha miwa ili ajenge kiwanda cha sukari kutokana na kujaa maji na kuharibu miundombinu eneo lote alilopewa hapo awali.

Mwekezaji huyo wa Kampuni ya SJ Sugar Distillery & Power Private amehakikishiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Geoffrey Mwambe aliyefanya ziara ya ghafla kwenda kujionea uharibifu mkubwa wa miundombinu ya eneo hilo kutokana na mvua kubwa zinazoendelea nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea eneo hilo la mwekezaji lililopo Kilambo, Mwambe alisema athari za mvua katika eneo la uwekezaji ni kubwa kutokana na zaidi ya miche 300,000 ya miwa kuharibika kwa sababu ya mafuriko katika eneo hilo.

“Wawekezaji hawa walishaanza kazi kwa kupanda miche kwenye eneo la ekari 500 kati ya hekta 3,000 walizopewa kufanya uwekezaji lakini eneo lote limeharibiwa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha,”alisema Mwambe.

Alisema TIC imefanya jukumu la kuwasiliana na Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kwa lengo la kumpatia eneo jingine mwekezaji ili aendeleze mradi wake ambao utakuwa na faida katika mikoa ya kusini na Taifa kwa ujumla.

“Tumeambiwa kiwanda kitakapokamilika kitaweza kuzalisha sukari tani elfu kumi, jambo ambalo litasaidia kupunguza uagizaji wa bidhaa hiyo nje ya nchi,” alisema Mwambe na kuongezea kuwa TIC itawajibika kikamilifu kuhakikisha mwekezaji anapata eneo lingine la kuwekeza mradi wake mapema iwezekanavyo.

Mwambe alisisitiza kuwa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli ni kujenga uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025 hivyo TIC ina wajibu wa kufanikisha azma hivyo inatimia pamoja na kumwezesha mwekezaji wa kiwanda cha sukari kunapatiwa eneo lingine la kuwekeza.

“Ipo haja kwa mwekezaji huyu kutafutiwa eneo mbadala la kufanyia uzalishaji kutokana na eneo la sasa kukumbwa na mafuriko hivyo kuathiri shughuli za uzalishaji,” alisema Mwambe.

HALMASHAURI ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma imehamasisha uzalishaji wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Mtwara

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi