loader
Picha

Eneo la Kanisa Anglikana latumika kukwepa kodi

ENEO la Kanisa la Anglikana lililopo Mtoni-Buza katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam limetumika kukwepa kodi ya pango la ardhi kwa kuendesha biashara vikiwemo viwanda vya Wachina na maduka makubwa.

Hayo yalibainika baada ya Mkuu wa Kitengo cha Kodi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Denis Masami kutembelea eneo hilo lenye jumla ya ekari 410 ambalo limemilikishwa kwa matumizi ya makazi na siyo biashara.

Masami alilazimika kufika katika eneo la taasisi hiyo baada ya kukaidi kulipa kodi ya pango la ardhi kwa muda mrefu kuanzia mwaka 2005 hadi sasa ambako maofisa ardhi kutoka Manispaa ya Temeke wamekuwa wakipeleka hati za madai mara nyingi bila ushirikiano wowote kutoka kwa taasisi hiyo.

Aidha, kwa mujibu wa mkuu huyo taasisi hiyo imebadili matumizi ya uendelezaji katika eneo hilo na wameweka wapangaji wanafanya biashara mbalimbali.

“Baadhi ya maeneo wameweka wapangaji na wamejenga kituo cha mafuta, maduka zaidi ya 200 na yote yanafanya biashara, gereji na viwanda vinavyozalisha bidhaa mbalimbali,” ilieleza taarifa ya Wizara ya Ardhi.

Hata hivyo, kutokana na shughuli zote hizi za kibiashara zinazofanywa katika eneo hili la kanisa, ni wajibu wao kulipa kodi ya pango la ardhi kwa kuwa linatumika kibiashara tofauti na taratibu za umilikishaji ambazo zilihusu eneo la ibada kitu ambacho sio cha kweli.

“Ikumbukwe kwamba tahere 27 Januari 2019 Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi alifuta kodi ya pango la ardhi kwa taasisi za dini na taasisi nyingine zinazotoa huduma, japo kuwa agizo hili halihusu taasisi zinazofanya biashara na kupata faida,” ilibainisha taarifa hiyo.

JAJI Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania, Dk Eliezer Feleshi amewataka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi