loader
Picha

Asakwa kwa kutupa pacha shimo la choo

POLISI mkoani Rukwa inamsaka mama aliyejifungua watoto pacha anayedaiwa kumtupa mmoja shimo la chooni.

Mzazi huyo anayedaiwa kujifungua pacha hao siku nne zilizopita anaishi Kijiji cha Namlengwa kilichopo katika Kata ya Lyowa katika Mji Mdogo wa Matai katika Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa. Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Justine Masejo alithibitisha mkasa huo ulitokea Machi 22, mwaka huu saa 1:00 asubuhi.

Akifafanua, alisema asubuhi hiyo ya tukio mkazi wa Kijiji cha Namlengwa, Veronica Maembe (55) akiwa amelala aligutushwa usingizini na sauti ya mtoto mchanga aliyekuwa akilia ndani ya shimo la choo nyumbani kwake.

“Uchunguzi wa awali wa kipolisi umebaini kuwa jirani na nyumba ya Veronika kulikuwa na mjamzito aliyejifungua watoto mapacha siku nne zilizopita...maofisa upelelezi wa polisi walipofika nyumbani kwake walikuwa nyumba iko wazi akiwa ameondoa kila kitu ndani. Maofisa wa polisi wanaendelea kumsaka mama huyo,” alieleza Masejo.

SERIKALI imesema katika mwaka wa fedha 2020/2021, imeweka mkazo katika ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi