loader
Picha

Tanroads yaweka lengo la kupanda miti 3,000

WAKALA wa Barabara Tanzania (Tanroads) mkoani Shinyanga umeweka malengo ya kupanda miti isiyopungua 3,000 kwenye hifadhi ya barabara huku ikitoa angalizo kwa baadhi ya wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kulima majaruba kandokando ya hifadhi watachukuliwa hatua.

Kaimu Meneja wa Tanroads Mkoa, Mibara Ndirimbi aliyasema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari, akieleza kuwa miti iliyopandwa zaidi kwenye hifadhi ya barabara ni ile ya kivuli sio ya matunda.

Alisema malengo ya kupanda miti 3,000 katika hifadhi za barabara ambapo mpango wa upandaji miti shughuli zake zilianza mwaka 2010 katika barabara za mjini Shinyanga hadi Maganzo na mwaka jana wamepanda miti kandokando ya babaraba ya Tinde kwenda Kagongwa hadi Kahama.

“Majaruba yaliyopo kwenye hifadhi za barabara yamekuwa yakiharibu matuta ya barabara sababu ya kutuama kwa maji na adui mkubwa wa uhalibifu wa barabara ni maji hivyo sipendi watu walime katika hiafdhi na waliolima watachukuliwa hatua maana ndio chanzo cha kutengeneza ajali,” alisema Ndirimbi.

Alisema kwa kushirikiana na Women Group waliendelea na mpango wa awamu ya pili ambayo walipanda miti katika hifadhi za barabara kutoka mjini Shinyanga kwenda Buhangija na awamu ya tatu iliendelea mpaka Tinde kwa kushirikiana na wananchi katika maeneo hayo.

Mhandisi wa Mazingira wa Tanroads mkoani Shinyanga, Rebeca Marando alisema mwaka jana walikuwa na mpango wa kupanda miti 5,000 lakini walifanikiwa kupanda miti 4,600 ambayo walishirikiana na wananchi kwa kuwagawia miti 400 kwa ajili ya kupanda kwenye maeneo yao.

Alisema ingawa miti 4,400 ilikaguliwa na kuonekana inastawi vizuri na mingine ilikufa kwa kuliwa na mifugo huenda kwa makusudi au bahati mbaya ikiwa Januari mwaka huu walifanikiwa kupanda miti 1,500 kutoka Old Shinyanga hadi Bubiki na kabla ya hapo kulikuwa na miti iliyopandwa 500.

Mshauri wa Misitu mkoani Shinyanga, Edmotti Billie alisema kwa Mkoa wa Shinyanga miti iliyopandwa ni 1,193,524 na kazi ilikuwa ikiendelea ya ufuatiliaji wa miti ya kupanda kutoka Mwadui lakini imesitishwa sababu ya Corona.

Billie alisema kutokana na Waraka Namba Moja wa Mwaka 2009 uliotolewa kutoka kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais kuwa halmashauri zipande miti kwa kukadiriwa, kiasi cha miti milioni 1.5 lakini zoezi limekuwa likisuasua kwa kutofikia malengo na kutopanga bajeti yake.

MAKUBALIANO ya mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ...

foto
Mwandishi: Kareny Masasy, Shinyanga

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi