loader
Picha

Wahamiaji 6, madereva 3 wanusurika kuuawa kwa kichapo

WAHAMIAJI haramu sita na madereva wa bodaboda watatu wamenusurika kuuawa na wananchi wa Kijiji cha Ibungu wilayani Ileje mkoani Songwe, baada ya kunasa kwenye mtego uliowekwa na wananchi hao.

Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo lililotokea Machi 25, mwaka huu, majira ya alfajiri kijijini hapo ni uvumi ulionea wa kuwepo watu wanaojihusisha na unyonyaji damu.

Baada ya taarifa hizo za kuonekana watu wanaodhaniwa ni wanyonya damu wakisafiri kwa kutumia pikipiki, inadaiwa wakazi hao waliweka kizuizi katika barabara kwa kupanga magogo jambo lililofanikisha kuwanasa.

“Tulipopata taarifa za kuonekana kwa watu wanaohisiwa ni wanyonya damu wanapita Kijiji cha Bupigu sisi tukajiandaa na kupanga magogo na mabenchi na baada ya muda mfupi tulifanikiwa kuwanasa, lakini baada ya kuwabana kwa kipigo walibainika kuwa ni wahamiaji haramu na walikuwa wakisafirishwa kwa njia ya panya kuelekea wilayani Kyela ili wavuke kwenda nchi jirani ya Malawi,” kilisema chanzo cha habari kijijini hapo.

KATIKA kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewasihi ...

foto
Mwandishi: Baraka Messa, Ileje

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi