loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Madaktari wapya ni neema kwa wagonjwa

SERIKALI imetangaza rasmi nafasi 1,000 za madaktari daraja la pili watakaojiriwa baada ya kibali chao cha ajira kutolewa rasmi na serikali.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dk Zainab Chaula amesema ajira hizo zinafuatia Rais Dk John Magufuli kukubali ombi lao la ajira.

Rais Magufuli alikubali ombi la madaktari kuongezewa nguvu kwa kuajiri watu 1,000. Dk Chaula akawaambia waandishi wa habari jijini Dodoma juzi kuwa, madaktari 610 watapelekwa hospitali zilizo chini ya Tamisemi. Pia akasema, madaktari 306 wataajiriwa hospitali za rufaa za mikoa zinazosimamiwa na wizara na wengine 40 Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Akaongeza kwamba madaktari 20 watapelekwa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma, 10 Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), 7 kwa ajili ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na 7 kwa ajili ya Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI).

Tumeguswa na hatua ya Rais Magufuli na pia serikali yake ya awamu ya tano kuona umuhimu wa kuajiri madaktari 1,000 hasa muda huu taifa linapokabiliana na homa ya virusi vya Corona.

Zaidi tumefurahishwa na mgawanyo mzuri wa wataalam hao wa matibabu ya aina mbalimbali na kuwataka watendaji wa taasisi hizo wawape ushirikiano mkubwa ili kuboresha huduma zao. Kwa muda sasa, taasisi nyingi za huduma za afya zimekuwa na uhaba mkubwa wa wataalam hivyo kuajiriwa kwa madaktari huo ni ahueni.

Ni ahueni kwa sababu itapunguza mzigo mzito ambao madaktari wamekuwa nao kuwahudumia wagonjwa na kufanya waombe ajira za wengine. Ni matarajio yetu kuwa, madaktari wapya wote watajitoa kwa dhati kuwahudumia wananchi kwa kujua kimsingi ndio waajiri wao wakuu.

Pia wajiandae kuwahudumia vizuri wakirejea kiapo chao cha utabibu na hivyo kufanya waone kuajiriwa kwao ni neema kutoka kwa serikali. Lakini tumefurahishwa zaidi na ujio wao muda huu kwa sababu nchi iko kwenye vita ya Corona hivyo tunatarajia ushirikiano wao mkubwa pia.

Wananchi wengi hivi sasa wanahitaji maelezo ya kina ya kujikinga na ugonjwa wa Corona na hivyo tunatarajia watashiriki kampeni hii pia.

WIKI hii kumekuwa na taarifa za Yanga kutakiwa ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi