loader
Picha

Uhuru wa kujieleza usitumike kupotosha jamii

UHURU wa kujieleza ni haki ya mwananchi yeyote raia wa Tanzania kulingana na Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoeleza kuwa kila mtu ana uhuru wa kujieleza, kwa kutoa maoni yoyote, kutoa mawazo yake na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote, bila ya kujali mipaka ya nchi na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.

Pia, inaeleza kuwa kila raia ana haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote, ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.

Kutokana na ibara hiyo, uhuru wa kujieleza unajumuisha haki ya kutoa mawazo au maoni ya aina yote, yawe ya kupendeza au kukosoa kwa lengo la kuhakikisha kila mmoja anakuwa huru kutoa maoni yake katika jambo lolote kuanzia ngazi ya familia, kazini na katika jamii na nchi kwa kuzingatia mipaka ya utoaji wa maoni yake.

Lakini ni dhahiri kuwa kutokana na haki hiyo, watu wamekuwa wakitumia vibaya uhuru huo, hususan katika mitandao ya kijamii, kwa kutoa maoni bila kujali athari ya jinsi walivyojieleza kwa jamii, ikiwa wanajenga au wanabomoa mustakabali wa nchi kwa kuhusisha masuala mbalimbali.

Wananchi wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, kutoa maoni yao ambayo wakati mwingine yanaweza kusababisha hofu, madhara na uchochezi miongoni mwa jamii na baadaye kusababisha tatizo kubwa bila kutarajia.

Nao wanasiasa kwa nyakati tofauti, wamekuwa wakitoa maoni au kutumia uhuru huu vibaya tofauti na lengo la kupewa uhuru huo, kwa kusababisha chuki kwenye jamii au kuchafua taswira ya nchi kimataifa. Ni dhahiri kwa kutumia uhuru huo, wanasiasa na wanaharakati wanaweza kukosoa masuala mbalimbali nchini kwa kutumia njia madhubuti zenye staha, huku wakihakikisha kauli zao hazileti madhara kwa jamii na kuacha kuendekeza umaarufu.

Licha ya kuwa ibara hiyo ya katiba inaelezwa kuwa haijawahi kutafsiriwa na mahakama ili kubainisha wigo wa uhuru wa kujieleza na wigo wa mipaka au masharti dhidi ya haki hii, ni vema katika hili kuhakikisha kila mmoja anaangalia madhara ya maoni yake kwenye jamii. Rai yangu ni kuwa uhuru huu wa maoni usitumike vibaya.

Mara nyingine watu wanatumia vibaya mitandao ya kijamii na vyombo vya habari rasmi wakijieleza au kutoa maoni, badala ya husababisa uchochezi katika jamii. Inaelezwa kuwa uchochezi, maana yake ni kujenga chuki au dharau au kuhamasisha manung’uniko dhidi ya utawala halali wa serikali.

Pia kuhamasisha wananchi kujaribu kubadilisha kwa njia isiyo halali jambo lolote nchini , kujenga chuki, dharau na kuamsha manung’uniko dhidi ya utoaji haki ndani ya Jamhuri ya Muungano. Lakini, pia kuamsha malalamiko na manung’uniko miongoni mwa watu au kundi la watu, kukuza hisia za uhasama na uadui baina ya makundi mbalimbali ya kijamii na mengineyo.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Arumeru imewafutia mashitaka washitakiwa ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi