loader
Picha

Mamia wamzika Dk Mahanga

MAMIA ya watu walijitokeza kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Ilala, Dk Milton Makongoro Mahanga, ambaye alizikwa jana katika makaburi ya Tabata Segerea, Dar es Salaam.

Dk Mahanga ambaye alizaliwa Aprili 3, 1955 alihamia Chadema mwaka 2015 akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM). Akiwa CCM alikuwa Mbunge wa Ukonga mwaka 2000-2010 na mbunge wa Segerea mwaka 2010-2015. Pia aliwahi kuwa nafasi mbalimbali katika baraza la mawaziri katika serikali ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Akizungumza msibani kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa chama hicho ambaye pia ni Mbunge wa Kibamba, John Mnyika alibainisha kuwa hadi kifo kinamkuta, Dk Mahanga amedhihirisha msimamo wake wa kisiasa.

Mnyika alisema,” Leo tunamuaga Dk Mahanga tukiwa tumekusanyika mahala hapa, licha ya tofauti zetu za kisiasa, kidini, kabila na tamaduni, na hii ni kutokana na kila mmoja kuguswa na kazi na upendo aliokuwa nao huyu bwana kwetu” Alisema, Dk Mahanga ana tofauti kubwa na wanasiasa wengine, ambao walihamia Chadema na kisha kurejea tena CCM, kwani yeye aliendelea kubakia Chadema akikipigania chama hicho.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally alisema kuwa Dk Mahanga alikuwa mwanasiasa aliyesimamia misimamo thabiti, yenye kujenga uimara wa chama na jamii kwa ujumla. Polepole alisema, Dk Mahanga ameacha somo kuwa licha ya tofauti za kisiasa nchini, bado wanasiasa wanapaswa kuheshimiana na kufanya kazi kwa bidii na sio kulaumiana na kupingana kwa kila kitu.

Alisema,”Leo tunamuaga mpambanaji huyu, ni vema tukatambua kuwa kwanza upendo na siasa za kweli ndio msingi wa maendeleo, na ndio maana kwa heshima yake leo tumekutana mahala hapa, licha ya tofauti zetu za kisiasa, lakini ni muda mzuri wa kuangalia uwezekano wa kuepuka maambukizi ya corona katika umati huu,” Aidha, mbali na viongozi hao, kila aliyepata nafasi ya kuzungumza kwenye msiba huo, aliweka mbele tahadhari ya maambukizi ya corona, ambapo hata wakati wa kuaga na kuchukua chakula, waombolezaji waliaswa kukaa umbali wa mita moja na kuepuka kugusana. Dk Mahanga ameacha mke Florence, watoto na wajukuu. Alifariki Machi 23, mwaka huu.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi