loader
Picha

TRC sasa wapakia abiria kulingana na viti

SHIRIKA la Reli Tanzania( TRC) limechukua hatua za kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona kwa abiria wanaosafi ri kwa treni zote za mjini na za mikoani. Sasa abiria hao wanakaa kulingana na idadi ya viti na kunawa mikono na maji, dawa na sabuni kabla ya kuingia ndani ya treni.

Aidha, TRC imeanza kupulizia dawa katika maeneo yote ya kazi kwenye stesheni zote za treni nchini, ikiwa ni pamoja na kutenga chumba ndani ya treni ziendazo mikoani kwa ajili ya kumhudumia abiria atakayebainika kuwa na dalili za ugonjwa huo, kisha atashushwa kwenye vituo vya afya jirani na stesheni.

Akizungumzia hatua hizo, Meneja wa Treni za Mjini na Mikoani wa TRC, Iddy Mzugu alisema hizo ni juhudi za kuunga mkono jitihada za serikali ,kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa corona, ukizingatia kuwa shirika linatoa huduma ya usafiri wa abiria wengi nchini. Alisema kuanzia Machi 18, mwaka huu, walianza kuwaelimisha wananchi na kuweka maji, dawa na sabuni kwenye stesheni zote kwa ajili ya abiria na wafanyakazi kunawa kabla ya kuingia kwenye treni.

Aidha, Machi 19, mwaka huu walianza utaratibu wa kupakia abiria kulingana na idadi ya viti kwa treni za jiji la Dar es Salaam ambazo hufanya safari kati ya Pugu na Kamata na Ubungo na Kamata, sambamba na kuongeza idadi ya ruti ili kuweza kubeba abiria wengi.

“Baada ya kutoa agizo kwamba treni zetu hazitapakia abiria wanaosimama, tuliona ni vyema pia tuongeze ruti kwa njia ya Pugu na Ubungo, badala ya zile za awali ambazo ni tatu asubuhi na tatu jioni sasa zimekuwa nne kwa kila ruti, ingawa tunapata changamoto kwa treni za mikoani”alisema Mzugu.

BAADHI ya mataifa yenye wagonjwa wengi na vifo vichache yameeleza ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi