loader
Picha

Ni nadra Olimpiki kupigwa kalenda

MASHINDANO ya Olimpiki 2020, imesogezwa mbele mpaka mwakani kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona (COVID-19) baada ya Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe kufanya kikao na Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC),Thomas Bach, Jumanne.

Inakadiriwa watu wapatao 10,000 walikuwa wameandaliwa kushiriki katika sherehe za ufunguzi wa michezo hiyo ya 32 zilizopangwa kufanyika katika Uwanja wa Taifa wa Tokyo. Pia watazamaji wapatao 600,000 kutoka mataifa mbalimbali walitarajiwa kwenda Japan kuhudhuria sherehe hizo pamoja na michezo hiyo, ambayo yalipangwa kufanyika kuanzia Julai 24 hadi Agosti 9 mwaka huu.

KUAHIRISHA

Kutokana na uwepo wa ugonjwa huu wa corona, kumefanya mashindano ya michezo mingi kuahirishwa duniani kote, yakiwemo Mashindano ya Mpira wa Magongo kwenye barafu 2020, Zurich pamoja na mbio za farasi za dunia, Dubai. Kuahirishwa kwa mashindano hayo ya Olimpiki kumekuja baada ya kuwepo kwa hofu kubwa juu ya hatari ya kusambaa kwa ugonjwa huu, ambao umeua watu wapatao 15,000 duniani kote mpaka kufikia Machi 23.

Machi 21, Bodi ya Wanariadha wa Marekani (USATF) imeisambaza barua waliyopewa juu ya kuahirishwa mashindano hayo na pia Kamati ya Olimpiki ya Norway na Brazil nao wametangaza rasmi.

Kutokana na hofu ya ugonjwa huu kuwa kubwa tangu awali, Canada walishatoa tamko la kutopeleka washiriki wake Tokyo kama michezo hiyo isingesogezwa mbele mpaka mwakani. Hii si mara ya kwanza Olimpiki kuahirishwa, mwaka 1940 ambapo ilipangwa kufanyika Septemba 21 mpaka Oktoba 6, 1940, Tokyo, Japan ilibidi ihamishiwe Helsinki, Finland, kuanzia Julai 20 mpaka Agosti 4, 1940, hata hivyo haikufanyika kutokana na Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Helsinki waliandaa Olimpiki ya mwaka 1952 na Tokyo mwaka 1964. Kuahirishwa kwa Olimpiki au kusogezwa mbele sio jambo rahisi, mzigo wa gharama wa kuiandaa michuano hii unakuwa juu ya Japan, ambayo imetumia takribani dola za marekani bilioni 12.6.

HASARA KUBWA

Kuahirishwa kwa michezo hiyo tayari kumeiingizia Japan hasara kubwa ya kiasi cha Sh trilioni 13 na huenda patp lake la taifa likaanguka kwa asilimia 1.4. Taarifa hii imewahuzunisha mno raia wa Japan, ambao walikuwa na tegemeo kubwa la kufaidika na mashindano hayo, mapaka Jumatatu iliyopita 70% ya raia wa nchi hiyo walikuwa wakiamini michezo hiyo kutosogezwa mbele.

Hii inatokea mara chache sana, tangu mfumo mpya wa Olimpiki ulivyoanza mwaka 1896, mara tatu tu ndiyo yameahirishwa. OLIMPIKI 1916 Ikiwa zimebaki siku kadhaa kuanza kwa Olimpiki ya mwaka 1916, Utawala wa Ujerumani wa wakati huo ulikuwa umepata hati ya kuwa mwenyeji baada ya kuipiku miji ya Alexandria, Amsterdam, Brussels, Budapest na Cleveland.

Mwaka 1913 maandalizi ya ujenzi wa uwanja wa kufanyika michezo hiyo ulikuwa tayari umeshakamilika ukiwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 30,000. Lakini haikufanyika baada ya kuibuka kwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Julai 1914. Ilitabiriwa kwamba vita vitamalizika mapema, lakini haikuwa hivyo vilidumu mpka Novemba 1918.

OLIMPIKI 1940, 1944

Ilipangwa kufanyika Tokyo na Sapporo, Japan ilipangiwa kuandaa Olimpiki ya majira ya joto na kiangazi kwa wakati mmoja mwaka 1940. Baada ya kuibuka vita kati ya Japan na China Julai 1937, serikali ya Japan iliamua kujitoa kuwa mwenyeji.

Mashindano yakahamishiwa Helsinki, Finland, lakini hayakufanyika baada ya kutokea kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Hali kama hiyo ilitokea katika mashindano ya mwaka 1944 iliyopangwa kufanyika London, England.

UONGOZI wa klabu ya Chelsea umempa ruhusa kiungo wake N’golo ...

foto
Mwandishi: TOKYO, Japan

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi