loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Takukuru wanastahili pongezi

KATIKA gazeti la HabariLEO jana, kulikuwa na habari ya Moto wa Takukuru sasa wahamia Iringa.

Ni habari iliyoeleza hatua zinazochukuliwa na taasisi hiyo mkoani humo ili kudhibiti rushwa.

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Iringa, Mweli Kilimali, wameokoa Sh 681,211,408 kutokana na uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha za Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo (Saccos).

Mweli anasema, fedha hizo zilizorejeshwa ndani ya miezi mitatu, ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa Sh bilioni 4.5 zilizofanyiwa ufisadi kwa Saccos 58. Alisema wamejielekeza zaidi katika kuchunguza kampuni za udalali zinazodaiwa kuvihujumu vyama vya ushirika kwa kukusanya fedha za madeni kutoka wadaiwa wao sugu na kuzila.

Tumefurahishwa na habari ya moto huo wa Takukuru kuhamia Iringa na kuungana na wananchi hasa wanyonge na pia vyama vya ushirika, Saccos kuomba wadau kuungana nao katika vita hii.

Pia tumefurahishwa zaidi na hatua ya Rais Dk John Magufuli kumpa rasmi, Ukurugenzi Mkuu Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo aliyekuwa akikaimu. Rais Magufuli alitangaza Ikulu, Dodoma wiki hii kuwa, kuanzia sasa Mbungo si kaimu tena bali ni Mkurugenzi Mkuu kufuatia mafanikio makubwa aliyopata tangu aongoze taasisi hiyo.

Alimsifu Mkurugenzi Mkuu huyo kwa kuokoa zaidi ya Sh bilioni nane za wakulima wa ufuta Lindi zilizokuwa zimeliwa na viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika (Amcos).

Mafanikio hayo ya Lindi yaliyosimamiwa na Brigedia Jenerali mwenyewe kufuatia agizo la Rais Magufuli alilotoa akiwa ziarani Lindi hivi karibuni na yale ya Iringa, yanaonesha utendaji wake na wa wasaidizi wake ulivyo wa makini.

Ni kwa msingi huo, tunaungana na Rais na pia wananchi wasiopenda rushwa kumpongeza tena Mbungo kwa kazi nzuri tukitaka wengi waige.

Kwa kurejesha zaidi ya Sh bilioni nane za Lindi Mbungo amethibitisha uwezo wake mkubwa na wa kupigiwa mfano na kustahili kuthibitishwa.

Ni matarajio yetu kuwa, Mbungo na watendaji wake wa Mkoa wa Iringa wataendeleza moto wa Lindi kwa kampuni za udalali zilizokosa Iringa.

Hatua yao iwe fundisho kwa kampuni nyingine nchini kufuata sheria zinapofanya kazi hasa zile zinazohusu maslahi ya wananchi wanyonge.

Kwa Amcos na wakulima wa Lindi, tunasema utapeli waliokuwa wamefanyiwa, uwe fundisho kwao katika kuchagua viongozi wenye maadili.

Si vizuri wakulima au wafanyakazi kuhadaiwa na kuchagua viongozi wasio waadilifu wakiwa na matumaini ya kuchukuliwa hatua na serikali.

Wahenga walisema kheri ya kinga kuliko tiba hivyo wachukue hatua ya kujihami na wizi huo na vitendo vya rushwa kwa kuchagua watu safi.

Kinyume chake, itakuwa ni kuitwika serikali mzigo mzito ambao ikitokea kuna uzembe wa kushughulikia, wataiona kama imewatelekeza. Tusifike huko, tuchukue hatua kuwadhibiti.

WIKI hii kumekuwa na taarifa za Yanga kutakiwa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi