loader
Picha

GSM kumrudisha Makambo Yanga

KLABU ya Yanga imeonesha jeuri ya fedha baada ya kuonesha nia ya kumrejesha aliyekuwa mshambuliaji wao, Heritier Makambo, huku wakijivunia mdhamini wao GSM kuwaunga mkono.

Makambo ni miongoni mwa majina yanayotajwa kipindi hiki na GSM wakitajwa wako tayari kununua mkataba wa mchezaji huyo anayetumikia Horoya FC ya Guinea kwa sasa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz, alisema watashirikiana na mdhamini huyo kuhakikisha wanaitengeneza Yanga kuwa ya kimataifa zaidi.

“Mdhamini wetu kwa kushirikiana na sekretarieti ya Yanga watafanya usajili mzuri kukijenga kikosi chetu kiwe cha ushindani, tunataka kuirejesha kauli mbiu yetu iwe Yanga ya kimataifa,” alisema.

Alisema si Makambo pekee, bali wanakusudia kufanya maboresho kwa kusajili wachezaji wengine wazuri kulingana na matakwa ya benchi la ufundi.

Makambo alicheza Yanga msimu mmoja uliopita na kuifungia mabao 17 na aliondoka mwaka jana kipindi ambacho klabu hiyo ilikuwa ikikabiliwa na ukata na kushindwa kumbakiza.

Hata hivyo, licha ya klabu hiyo kuendelea kumtegemea mdhamini huyo katika masuala ya usajili ujao, bado wenyewe baada ya kuandika barua ya kujitoa katika masuala yaliyoko nje ya mkataba hawajajitokeza hadharani kuzungumzia tena hatua waliyofikia.

Hivi karibuni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Hersi Said, alisema wanasubiri barua ya Yanga waweze kuzungumza na tayari klabu hiyo imesema imejibu barua hiyo.

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji waliokuwa wametajwa kuwa ni chanzo cha wadhamini hao kujiondoa katika baadhi ya majukumu walijiuzulu, wakiwemo Rogers Gumbo, Shija Richard na Mwalimu Kambi, huku Salum Rupia na Raphael Kamugisha wakisimamishwa.

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Simba, raia wa Burundi, Meddie Kagere ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi