loader
Picha

Mwakyembe: Maandalizi ujenzi uwanja wa Dodoma yanaendelea

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema serikali inaendelea na mawasiliano baina yake na serikali ya Morocco kuhusu kukamilisha mradi wa ujenzi wa uwanja wa michezo.

Dk Mwakyembe aliyasema hayo jana wakati wa kujibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Felister Bura (CCM) aliyetaka kujua ni lini uwanja wa michezo utaanza kujengwa kutokana na serikali kupata ufadhili kutoka serikali ya Morocco.

Akijibu swali hilo, Dk Mwakyembe alisema: “ Mfalme Mohamed VI alipofanya ziara yake Tanzania Oktoba, mwaka 2016 alitoa ahadi ya kufadhili miradi mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa msikiti na uwanja wa kisasa wa michezo. “Baadhi ya ahadi kama ujenzi wa msikiti zimekamilika.” Dk Mwakyembe alisema serikali iliamua uwanja huo ujengwe katika Jiji la Dodoma eneo la Nane Nane.

Alisema maandalizi yote ya msingi ikiwa ni pamoja na kutenga eneo lenye ekari 328.6, kupima eneo lote la mradi, kufanya tathimini ya mazingira na kijamii na kuandaa mchoro wa awali wa uwanja tarajiwa yamefanywa. “Kimsingi maandalizi ya awali ambayo yalipaswa kufanywa na serikali ya Tanzania yamekamilika kwa kiasi kilichokusudiwa.

“Pia mawasiliano baina ya serikali mbili za Tanzania na ile ya Morocco kuhusu kukamilisha mradi huu yanaendelea.

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Simba, raia wa Burundi, Meddie Kagere ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi