loader
Picha

Wahamiaji haramu watozwa dola 16,000

WAHAMIAJI haramu 65 kutoka mataifa mbalimbali wamekamatwa mkoani Shinyanga kwa kuingia nchini kinyume cha sheria za uhamiaji na kutozwa dola za Marekani 16,000.

Naibu Kamishina wa Uhamiaji mkoani hapa, Rashidi Magetta amesema wahamiaji hao walikamatwa katika operesheni maalumu iliyofanyika katika wilaya zote za mkoa huo kuanzia mwishoni mwa Desemba mwaka jana.

Magetta akizungumza na waandishi wa habari alisema miongoni mwa watuhumiwa wamo waliokamatwa kwa kuishi nchini bila kibali. Alisema watuhumiwa 65 wametozwa dola 600 kila mmoja ikiwa ni ada ya kibali maalumu cha muda cha kuishi nchini kwa miezi mitatu na baada ya muda kumalizika watarudishwa kwao.

Kati ya watuhumiwa waliokamatwa kwa kutokuwa na vibali vya kuishi, watuhumiwa 10 ni raia kutoka China, wanane kutoka India, watatu Afrika Kusini, Zimbabwe wawili, Ujerumani mmoja na Syria mtuhumiwa mmoja.

Kamishna huyo alisema kati ya waliokamatwa wapo walioingia nchini bila ya kuwa na kibali na wanaoajiriwa kufanya shughuli za kilimo katika mashamba ya tumbaku kata za Ushetu na Ulowa wilayani Kahama mkoani Shinyanga. Mbali ya waliokamatwa kwa kutokuwa na vibali vya kuishi nchini, 38 walikamatwa kwa kuingia kinyume cha sheria za uhamiaji na kurudishwa kwao, 32 kutoka Burundi, 4 Rwanda, 2 Kenya.

“Tunaendelea kuwasaka wahamiaji haramu maeneo yote ya mkoa ikiwemo wale wanaoingia nchini kwa njia za panya. Serikali imetoa agizo la kuimarishwa misako hasa maeneo yote yenye viashiria vya kuingia wahamiaji haramu kipindi cha ugonjwa wa corona, Covid-19,” alisema.

Magetta alisema miongoni wa watuhumiwa wamo wanawake watatu ambao si raia ambao wameolewa na wanaume wa kitanzania bila ya kufuata taratibu za kuwapatia hati ya kuishi ambao hata hivyo wote wametekeleza na kuruhusiwa kuendelea kuishi na waume zao. Kamishina huyo alisema idara yake bado ina changamoto kutekeleza operesheni ikiwemo uhaba wa vyombo vya usafiri kufikia maeneo mengi zaidi na baadhi ya wamiliki wa nyumba za kulala wageni kuwaficha wahamiaji haramu.

WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imeweka mkakati wa upatikanaji wa ...

foto
Mwandishi: Kareny Masasy, Shinyanga

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi