loader
Picha

Diamond, meneja wake watoka karantini ya Corona Dar

Mwanamuziki Diamond Platnumz na meneja wake, Sallam SK wameruhusiwa kutoka ‘’karantini’ baada ya kutiliwa shaka kuwa wameambukizwa virusi vya Corona.
Diamond ameweka wazi barua iliyoandikwa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dk Samuel Laizer katika ukurasa wake wa Instagram na kuandoka maneno yaliyosomeka: 
“Namshukuru Mwenyez Mungu. Tumemaliza salama siku 14 chini ya Uangalizi Maalum wa Madaktari na hatujakutwa na tatizo lolote la CORONA.... 
“Na sasa tunaingia rasmi mtaani kwa jili ya kuendelea kuijenga nchi yetu... Nawasihi ndugu zangu tuweni makini sana maana Corona ipo na INAUA.. tujitahidi kufuata ushauri tunaoelekezwa.” 
Naye SK amesema kwa sasa yupo ‘fit’ kurejea kwenye shughuli zake za kila siku huku akiomba Watanzania kuendela kuchukua tahadhari dhidi ya virusi  hivyo. 
“Nimshukuru Allah na wote mlionitumia msg, comments, DM na dua zenu. Bila kuwasahau Temeke Isolation Centre kwa kuwa bega na bega pamoja na mimi bila kunichoka pale nilipokuwa nimezidiwa na shukrani zangu nyingine ziende kwa madaktari bingwa kujua maendeleo yangu mara kwa mara…..” aliandika meneja huyo.

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Simba, raia wa Burundi, Meddie Kagere ...

foto
Mwandishi: Na Tagato James

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi