loader
Picha

Benki ya Dunia kujenga mahakama za wilaya 33

BUNGE limeelezwa kuwa ujenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya Uyui ni miongoni mwa majengo ya mahakama za wilaya 33 yaliyopangwa kuanza kujengwa Juni mwaka huu kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.

Hayo yamebainishwa bungeni leo katika majibu yaliyotolewa na Wizara ya Katiba na Sheria kwenye swali la Mbunge wa Tabora Kaskazini, Almasi Maige (CCM).

Maige amesema: “Wilaya ya Uyui haina Mahakama ya Wilaya na ina mahakama moja tu ya mwanzo inayotumia chumba kidogo katika Jengo la Mkuu wa Wilaya ya Uyui baada ya kutelekeza Mahakama ya Mwanzo ya Upuge.”

Hivyo ametaka kujua ni lini serikali itajenga mahakama ya wilaya ya Uyui, pia ametaka kujua ni kwa nini serikali ilitelekeza Mahakama ya Mwanzo ya Upuge pamoja na majengo yake katika Kijiji cha Upuge.

Katika majibu ya wizara hiyo, yameeleza kuwa uhaba wa majengo ni moja ya kero kubwa inayoikabili Mahakama ya Tanzania na mahitaji ya majengo ya kuendeshea shughuli za Mahakama nchini ni makubwa.

“Kwa msingi huo, Mahakama imejiwekea utaratibu wa kujenga majengo haya kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha, lakini ujenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya Uyui ni miongoni mwa majengo ya mahakama za wilaya 33 yaliyopangwa kuanza kujengwa mwezi Juni, 2020,” ilijibu wizara.

Pia imebainisha kuwa kwa sasa mahakama ipo katika hatua za mwisho kukamilisha mchakato wa awali ili ujenzi wa majengo hayo uanze kwa muda kama ilivyo katika mpango wa mahakama.

Serikali pia haikulitelekeza Jengo la mahakama ya mwanzo Upuge, sababu kubwa ilikuwa ni uchakavu wa jengo lenyewe ambalo halikuwa rafiki kuendelea kutumika kuendeshea shughuli za mahakama.

Hata hivyo, wizara ilishukuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Uyui kwa kuwezesha kupata ofisi kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma za Mahakama ya Mwanzo Upuge wakati taratibu za ujenzi wa Jengo la Mahakama ya Wilaya zikiendelea.

MTANDAO wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia (MKUKI) umesema wasichana 40 ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi