loader
Picha

Halmashauri zote kufikiwa na Tasaf

BUNGE limeelezwa kuwa kipindi cha pili cha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini utatekelezwa katika halmashauri zote 185 za Tanzania Bara na wilaya zote za Zanzibar zikiwamo zile ambazo hazikufi kiwa kipindi cha kwanza.

Hayo yalielezwa kwenye majibu yaliyotolewa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kutokana na swali la msingi la Mbunge wa Lupembe, Joram Hongoli.

Katika swali lake hilo, Hongoli alitaka kujua ni lini serikali itaingiza kaya zote ambazo hazikuingizwa kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF). Utekelezaji wa kipindi cha pili utatekelezwa katika vijiji, mitaa na shehia zote ikiwa ni pamoja na zile ambazo hazikufikiwa katika kipindi cha kwanza.

Katika kipindi cha kwanza cha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilitekelezwa kwa miaka sita kuanzia mwaka 2013 hadi 2019. “Rasilimali zilizokuwepo zilitosheleza kufikia Vijiji/Mitaa/ Shehia 9,960 ambazo ni sawa na asilimia 70. Katika Kipindi hiki jumla ya Vijiji/Mitaa na Shehia 5,590 nchini kote hazikufikiwa.

“Ninapenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa kipindi cha Pili cha Mpango huu kimezinduliwa rasmi tarehe 17 Februari, 2020 na Rais John Magufuli,” alieleza.

“Wakati wa uzinduzi wa Kipindi cha Pili, Rais aliagiza kufanyika kwa uhakiki wa walengwa wenye sifa za kuwemo kwenye Mpango huo, kuhakikisha kaya zote zenye watu wenye uwezo wa kufanya kazi wanafanya kazi na kulipwa ujira katika miradi ya kuboresha miundo mbinu ya afya, elimu na maji na kutoa elimu kwa walengwa ili kutumia ruzuku wanazopata kujikita katika kuzalisha na hatimaye kuacha kutegemea ruzuku,” alieleza.

CHAMA cha ADA- Tadea kimesema kitendo cha Mbunge wa Kawe, ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi