loader
Picha

Zatengwa bilioni 5/- kujenga barabara ya Same-Mkomazi

MBUNGE wa Same Mashariki, Naghenjwa Kaboyoka (Chadema), amehoji serikali ina mkakati gani wa kutimiza ahadi ya Rais ya kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya Same – Kisiwani hadi Mkomazi ambayo inaunganisha majimbo matano.

Akiuliza swali bungeni jana, mbunge huyo alisema barabara hiyo inaunganisha jimbo la Same Magharibi, Same Mashariki, Mlalo, Mkinga na Korogwe Vijijini.

“Je, ni fedha kiasi gani zimetumika kuanzia mwaka 2015/2016 – 2019/2020 kwa ajili ya kukarabati barabara hiyo,” alihoji Kaboyoka.

Katika majibu ya Wizara aya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, yameelezea kuwa barabara hiyo imekuwa ikifanyiwa matengenezo ya aina mbalimbali kila mwaka. Aidha, kuanzia Mwaka wa Fedha 2015/16 hadi 2019/20, kiasi cha Sh bilioni 3.29 kimetumika kwa ajili ya matengenezo mbalimbali ya barabara hiyo.

“Kufuatia kufanyika na kukamilika kwa upembuzi yakinifu pamoja na usanifu wa kina kwa kilometa zote za barabara hiyo kilometa 100.5,” ilieleza wizara.

Hata hivyo, serikali kupitia wizara hiyo imetenga kiasi cha Sh bilioni tano katika mwaka wa fedha 2020/21 ili kitumike kuanza ujenzi kwa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.

CHAMA cha ADA- Tadea kimesema kitendo cha Mbunge wa Kawe, ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi