loader
Picha

Wafanyabiashara waonywa kujenga juu ya mitaro

OFISA Masoko wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, James Yuna amewataka wafanyabiashara katika masoko mbalimbali jijini hapa kuacha kujenga vibanda juu ya miundombinu ya mifereji.

Yuna alitoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Sabasaba. Alisema ujenzi wa vibanda juu ya miundombinu ya maji kuna vuruga mwelekeo wa maji na kuyafanya kuzagaa.

Ofisa huyo aliwataka waliojenga juu ya mitaro ya kupitishia maji taka kwenye masoko yote ya ndani ya jiji hilo kuhakikisha wanajiondoa wenyewe ili waweze kunusuru mali zao.

Yuna alisema mpango wa Halmashauri ya Jiji ni kuona wafanyabiashara wake wanainuka kiuchumi kupitia biashara zao, siyo kuwaona wakikiuka sheria na taratibu katika kujipatia kipato.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka Ngumu Jiji la Dodoma, Dickson Kimaro alisema kitendo cha wafanyabiashara kujenga juu ya miundombinu inayopitisha maji pia kunasababisha kushindwa kufanyika kwa usafi kwa wakati.

Alisema mitaro ya maji inatakiwa kuwa wazi muda wote ili kuweza kubaini ni wapi kunatakiwa kufanyiwa usafi kwa kuondoa taka ngumu, lakini kitendo cha kujenga juu ya mitaro hiyo kunasababisha kuziba mitaro na kusababisha maji kuzagaa ndani ya soko.

Alisema hivi sasa kwa mvua zinazoendelea kunyesha Jiji kamwe haiwezi kuruhusu hii hali iendelee kwa kuzagaa maji na takataka kila kona kutokana na mitaro kuziba.

WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imeweka mkakati wa upatikanaji wa ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi