loader
Picha

Buriani Marin Hassan Marin 1972-2020

“JANA usiku tulikuwa naye kwenye kipindi cha Ardhio mpaka mwisho kilipoisha saa tatu usiku, na baada ya kipindi tulifanya kikao cha mapitio kuangalia wapi pa kuboresha, na kupanga kipindi kingine cha Ardhio leo (jana) ambacho kinaruka ndani ya saa 120 hewani.

“Tulitoka tukiwa tunacheka na bashasha getini na tuliingia kwenye gari tukaenda naye na kumshusha nyumbani kwake, ameondoka kwenye geti hili (la ofisi za TBC), akiwa anatembea, leo anaingia kwenye geti hili yupo kwenye jeneza,” alisema Florence Mavindi kwa sauti ya kutetema yenye kiashiria cha machozi ndani yake.

Mtangazaji huyo wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) alitoa kauli hizo huku akilia wakati akijiandaa kuaga mwili wa mtangazaji nguli na mahiri wa TBC1, Marin Hassan Marin aliyeaga dunia ghafla jana asubuhi. Marin aliyejijengea jina kubwa kwa utangazaji wa simulizi, alifariki dunia ghafla jana saa 2:55 asubuhi kwenye Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam, chini ya saa 24 tangu amalize jukumu lake la kazi Jumanne usiku.

Magufuli atoa ndege yake

Kutokana na kifo hicho, Rais John Magufuli alituma salamu za rambirambi ikiwa nipamoja na kutoa ndege yake kubeba familia ya Marin kutoka Dodoma hadi Dar es Salaam ambako pia ilitafutwa ndege maalumu ya kubeba maiti na kwenda Zanzibar kwa maziko yanayofanyika leo katika makaburi ya Mwanakwerekwe.

Katika salamu hizo, Rais Magufuli alisema: “Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko taarifa za kifo cha ghafla cha mtangazaji maarufu na mahiri, Marin Hassan kilichotokea leo (jana) jijini Dar es Salaam. Naye mtangazaji wa TBC1 ambaye alifanya kazi kwa karibu na Marin, Elisha Eliah akimuelezea alisema alikuwa mwalimu, alikuwa ni mbunifu na anayejenga hoja na kuzitetea, na alikuwa sio mtu wa kukata tamaa.

“Kuna mazingira unaweza kuona hapa tumeshindwa lakini Marin alikuwa hakubaliani na hilo jambo mpaka litimie, kuna wakati alikuwa anauliza katika kufanikisha hili kuna jambo gani ulikwama, hili usifanye, hili fanya hivi, nilitamani katika utendaji wangu niendelee kujifunza mambo mengi zaidi,” alisema Eliah.

Samia, Majaliwa wamlilia

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akitoa pole kwa familia na waandishi wote kutokana na kifo hicho, alisema, “Kwa masikitikio na mshtukio nimepokea taarifa ya kifo cha mwandishi wa habari mwandamizi, mtangazaji na mbunifu wa vipindi mbalimbali wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), namuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.”

Kwa upande wake, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimuelezea marehemu Marin alisema, “Kifo chake nimekipokea kwa mshtuko mkubwa, Marin alikuwa ni kijana aliyependa kazi yake, aliyebobea katika nyanja zote hasa siasa, Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi.”

Mwakyembe: Ni pigo kubwa

Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alieeleza kuwa TBC na tasnia ya habari kwa ujumla imepata pigo kwani Marin alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha sekta ya habari inakuwa na mchango chanya katika maendeleo ya jamii. Dk Mwakyembe ametoa pole kwa familia, ndugu,jamaa,marafiki na wadau wote wa tasnia ya habari nchini.

Kipindi cha Kishindo Ardhio

Eliah alisema miongoni mwa vitu walivyozungumza na Marin juzi alimpa maagizo ya kutengeneza kitu ambacho kitawasilisha mikoa 18 na iwe ‘clip’ ya dakika mbili ambayo itazungumzia kila kitu ikiwemo kilimo, siasa, elimu.

“Kaniachia mzigo, sijui sasa nitamuliza nani alikuwa anataka kiweje, katika miezi mitatu ya ardhio,” alisema.

Kuhamia Dodoma

Mwaka 2018 wakati Serikali ya Awamu ya Tano ipo kwenye harakati za kuhamia Dodoma, Marin alikuwa mstari wa mbele kuandaa vipindi mbali mbali ambavyo vilielezea safari ya kwenda Dodoma. Kibwagizo cha kipindi chake kilikuwa ‘Jamaniii Dodomaaa, Dodoma ya Watanzania, Dodoma yapendeza,” na kuonesha matukio mbali mbali ya serikali kuelekea Dodoma ikiwa ni pamoja na kuwahoji viongozi wa serikali.

Baadhi ya vipindi ambavyo aliviasisi pia siku za nyuma ni Kipindi cha Darubini wakati TVT ipo kwenye mchakato wa kuingia TBC na baadaye Kipindi cha Nyumba ya Jirani na Kapu la TBC ambacho kinaendelea hadi sasa.

Alisema Marin kama muasisi wa kipindi kipya cha urushaji habari kilichopewa jina la ‘Ardhio’ Jumamosi wakiwa kwenye harakati za uzinduzi wa kipindi hicho, aliwaasa msamaha pale wanapogombana, ushirikiano na kubebeana madhaifu yao.

“Alikuwa anapenda sana kusisitiza tupende kujifunza, tujifunze kwa kuona, kujifunza darasani na kutenda. Ardhio upashaji mpya wa habari na ukweli usiopingika tunatembea juu ya mawazo yake,” alisema Zakaria akirejea uzinduzi huo Marin alishindwa kuendelea kuzungumza na kulia wakati akihoji baada ya uzinduzi. Korido za TBC Katika korido za TBC ilikuwa ni vilio na majonzi, wanaume kwa wanawake, vijana walionekana kulia zaidi na kuomboleza kwa tafsiri kuwa taa imezimika.

Mwili kuwasili TBC Saa 6:31 mchana jana, mwili wa Marin Hassan Marin uliingia ndani ya Ofisi za TBC Mikocheni kwa ajili ya wafanyakazi wenzake kumuaga. “Mwenyewe alikuwa anasema tutapita hewani 360, lakini amekwenda kwa saa 140 hakuweza kufika alikodhamiria. Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Matukio, Frank Bahati alisema, “Leo (jana) majira ya kumi na mbili asubuhi ndugu yetu Marin alimpigia simu dereva na kumwambia anajisikia vibaya, kwa taarifa ni kwamba alipopata tatizo majira ya saa 12 asubuhi alijisikia vibaya…majirani wakampeleka hospitali na kumpeleka Lugalo, majira ya saa tatu kasoro ndugu yetu akafariki.”

Wasifu wa Marian

Marin Hassan Marin alizaliwa mwaka 1972 katika Kijiji cha Banda Maji katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, kwa baba na mama wakiwa na asili ya Comoro. Alimaliza elimu yake ya sekondari mwaka 1992 Shule ya Sekondari Haile Selassie, na baadaye aliajiriwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC. Aliwahi kufanya kazi katika vyombo mbali mbali vya habari Kenya hususani KTN

CHAMA cha ADA- Tadea kimesema kitendo cha Mbunge wa Kawe, ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi