loader
Picha

Benki ya dunia yaipa Tanzania trilioni 1.1/- mapinduzi ya elimu

MAPINDUZI makubwa yanatarajiwa kufanyika katika sekta ya elimu nchini kutokana na mkopo wa gharama nafuu wa Dola za Marekani milioni 500 (takribani Sh trilioni 1.135) zilizoidhinishwa na Benki ya Dunia kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuimarisha sekta hiyo.

Taarifa iliyotolewa leo na benki hiyo imesema mkopo huo utawezesha mamilioni ya vijana kupata na kuhitimu elimu ya sekondari katika mazingira bora ya kusomea, na imeahidi kuendelea kujadiliana na serikali kuhusu masuala ya elimu.

“Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango tumeupokea kwa mikono miwili uamuzi wa Benki ya Dunia wa kuidhinisha kiasi hicho cha mkopo nafuu,” Msemaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Benny Mwaipaja.

Mwaipaja amesema fedha hizo kupitia Mradi wa Maboresho ya Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) zitasaidia kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu nchini kwa kuongeza ubora wa elimu kwa kuimarisha elimu ya watoto wa kike na wa kiume kwa sababu watajengewa mazingira mazuri ya miundombinu ya elimu.

Amesema wajibu wa wizara ni kuhakikisha fedha zitakapo kuja zinatumika vizuri na kwa malengo yaliyokusudiwa kupitia Wizara Elimu, Sayansi na Teknolojia. Uamuzi wa benki kupitia Chama cha Maendeleo ya Kimataifa (IDA) unatajwa kuwa ni wa kihistoria ikizingatiwa shinikizo kutoka kwa baadhi ya wanaharakati nchini na wa kimataifa waliokuwa wakiitaka benki isitoe mkopo kwa Tanzania wakidai kwamba ina sera na sheria ya elimu ya kibaguzi.

 

MTANDAO wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia (MKUKI) umesema wasichana 40 ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi