loader
Picha

Mmoja aongezeka,wawili wapona corona

IDADI ya wagonjwa waliothibitika kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (Covid-19) imeongezeka na kufi kia 20, baada ya mtu mmoja kubainika kuwa na virusi hivyo nchini, lakini mmoja kati ya waathirika akipona.

Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, mgonjwa huo mpya alipatikana jijini Dar es Salaam na ni raia wa Marekani, mwanamke mwenye umri wa miaka 42.

“Raia huyu amekuwa karibu na mtu aliyesafiri nje ya nchi na baadaye kuthibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona aliporejea nchini,” alisema Ummy.

Alisema hadi sasa jumla ya kesi za maambukizi ya ugonjwa huo ni 20 ambapo wagonjwa 17 wanaendelea vizuri na matibabu. Aidha, alisema hadi juzi mmoja kati ya wagonjwa waliokuwa katika Kituo cha Matibabu cha Temeke Dar es Salaam amethibitika kupona maambukizi aliyokuwa nayo na ameruhusiwa kurudi nyumbani na hivyo kufanya jumla ya watu waliopona kuwa wawili.

Juzi, serikali ilitangaza kifo cha kwanza cha mtu aliyefariki na ugonjwa wa Covid 19 nchini ambaye ni Idd Mbita (49) aliyezikwa na serikali huku ndugu zake wachache wakiruhusiwa kushiriki maziko hayo.

Mtandao wa worldometer hadi jana mchana ulionesha kuwa tangu maambukizi ya virusi vya corona yaingie duniani, jumla ya watu 877,580 wamepata maambukizi, watu 43,569 wamepoteza maisha na watu 185,065 wamepona.

Aidha, kwa siku ya jana pekee hadi mchana kulikuwa na maambukizi ya virusi vya corona kwa watu 19,261 na vifo 1,267 huku Hispania ikiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu waliopoteza maisha waliofikia 589 na maambukizi 6,213.

Nchi nyingine zinazofuatia kwa maambukizi na vifo ni Iran yenye watu 138 waliopoteza maisha kwa siku ya jana pekee huku maambukizi yakifikia watu 2,988 na Belgium vif

MTANDAO wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia (MKUKI) umesema wasichana 40 ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi