loader
Picha

Majaliwa: Mwenye corona apelekwe eneo la maalumu bila kujali cheo

WATANZANIA wametakiwa kuzingatia masharti ya afya na atakayethibitika ni mgonjwa, ikatangazwa kuwa ana virusi vya corona ni lazima bila kujali cheo chake awe waziri, katibu mkuu au mkurugenzi atalala palipoandaliwa.

Hayo yalisemwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana wakati akiwasilisha hotuba yake kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2020/2021.

“Niwatake Watanzania kuzingatia masharti ya afya kwa kufuata ushauri unaotolewa na Serikali, mgonjwa akithibitika, kutangazwa ni lazima bila kujali cheo chake, awe Waziri, Katibu Mkuu au Mkurugenzi atalala palipoandaliwa. Watanzania wenzangu tuendelee kupuuza taarifa za uzushi zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii,” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu alifafanua kuwa hivi sasa nchi na dunia kwa ujumla inapitia katika kipindi kigumu na kuwa itakumbukwa kwamba, Machi 11, 2020, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza mlipuko wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona (COVID-19) kuwa ni janga la Kimataifa.

Aidha, Machi 16, 2020 serikali ilitangaza kuwepo kwa mgonjwa wa kwanza nchini. Alisema tangu kugundulika kwa ugonjwa huo, serikali inachukua hatua mbalimbali kukabiliana na janga hilo ikiwamo kuimarisha ukaguzi na ufuatiliaji wa wasafiri wanaoingia nchini ili kubaini wasafiri wanaoonesha dalili za ugonjwa au wenye viashiria hatari.

CHAMA cha ADA- Tadea kimesema kitendo cha Mbunge wa Kawe, ...

foto
Mwandishi: Angela Semaya, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi