loader
Picha

Serikali yataka siasa za kistaarabu uchaguzi mkuu

KATIKA kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewasihi viongozi wa vyama vya siasa kuonesha mfano wa kuendesha siasa za kistaarabu zenye lengo kuwaunganisha Watanzania na si kuwatenganisha.

Pia amewasihi wananchi kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi mkuu ujao uliopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi. Waziri Mkuu Majaliwa ametoa rai hiyo jana bungeni alipokuwa akielezea hali ya kisiasa wakati wa kusoma hotuba ya makadario ya mapato na matumizi kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2020/2021.

Alisema hakuna kiongozi aliyewahi kupata sifa nzuri kwa kuwa chanzo cha mafarakano na hivyo kutumia fursa hiyo kuwasihi viongozi hao kuwa mfano.

“Niwasihi Watanzania kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi mkuu ujao kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi,” alisema Waziri Mkuu.

Aliongeza, “Kwa viongozi wa vyama vya siasa waoneshe mfano wa kuendesha siasa za kistaarabu zenye lengo la kuwaunganisha Watanzania na sio kuwatenganisha. Hakuna kiongozi aliyewahi kupata sifa nzuri kwa kuwa chanzo cha mifarakano.

“Hivyo basi, tudumishe utulivu, amani, mshikamano pamoja na ustaarabu wetu wa kitanzania katika kipindi chote cha kampeni na uchaguzi mkuu ili kulifanya taifa letu kuendelea kuwa kisiwa cha amani na mfano wa kuigwa barani Afrika na duniani kwa ujumla.”

Aidha, alisema Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeendelea kusimamia utekelezaji wa maadili ya vyama vya siasa ili kuhakikisha demokrasia ya vyama vingi inaimarika pamoja na kudumisha amani, utulivu na mshikamano uliopo.

“Katika mwaka 2020/2021, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa itaendelea kusimamia utekelezaji na utoaji elimu kuhusu Sheria ya Vyama vya Siasa, Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa, pamoja na Sheria ya Gharama za Uchaguzi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

CHAMA cha ADA- Tadea kimesema kitendo cha Mbunge wa Kawe, ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi