loader
Picha

Pamoja na corona watu wapewe haki zao-Jaji Kiongozi

JAJI Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania, Dk Eliezer Feleshi amewataka mahakimu na watumishi wa Mahakama kwa ujumla kuendelea kuhudumia wananchi licha ya changamoto ya janga la corona kutikisa dunia kwa sasa.

Akizungumza kwa nyakati tofauti alipotembelea mahakama kadhaa jijini Dar es Salaam juzi, Jaji Dk Feleshi alisema kuwa kila hakimu ajikumbushe wajibu wake kwa kusoma vifungu 107A na B vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vilevile wakumbuke kusimamia viapo vyao.

“Kipindi kama hiki hakisimamishi migogoro kutokea kwenye jamii, hivyo ni lazima kazi zifanyike, ni kipindi ambacho kinatukumbusha ni namna gani bora zaidi ya kuboresha huduma ya utoaji haki nchini,” alieleza.

Aliwataka watumishi hao kuwa wabunifu katika maeneo yao ya kazi na kutokubweteka kwa kusikiliza idadi chache ya mashauri kwa Mahakama ambazo zina idadi chache ya mashauri na kuwataka kutosita kudai nyongeza ya idadi ya mashauri ya kuyafanyia kazi endapo waliopangiwa na wafawidhi wao ni machache.

Aidha, aliwataka mahakimu wafawidhi wa Mahakama za Wilaya ya Kigamboni, Temeke na Ilala kuendelea kuboresha ushirikiano na wadau wa Mahakama katika kuhakikisha kuwa haki inatolewa kwa wakati.

CHAMA cha ADA- Tadea kimesema kitendo cha Mbunge wa Kawe, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi