loader
Picha

Mwanri afuta likizo maofisa afya wazuie corona

MKUU wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amesimamisha kwa muda likizo za watumishi wakiwemo wa Idara ya Afya ili waendelee kuunganisha nguvu kusaidia jamii kampeni dhidi ya virusi vya corona.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuna wataalamu wa kutosha maeneo yote watakaoendelea kutoa elimu ya kujikinga na kudhibiti ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na corona usiingie Tabora.

Mwanri alitoa kauli hiyo jana Uyui na Nzega wakati wa ziara ya kagua vituo na zahanati zilizoandaliwa kwa ajili ya washukiwa wa ugonjwa wa Covid -19 kama itatokea bahati wakaonekana mkoani humo.

Alisema kipaumbele hivi sasa ni kuhakikisha tahadhari zote zinachukuliwa ili wakazi wa Mkoa wa Tabora waendelee kuwa salama kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu na viongozi wa kitaifa.

Mwanri alizitaka halmashauri zote za Mkoa wa Tabora kutumia redio zilizopo na magari ya matangazo kupeleka elimu katika maeneo mbalimbali ya wananchi juu ya kujikinga na kulinda dhidi ya Covid -19.

“Tumieni magari yenye vipaza sauti kupitia katika mitaa mbalimbali kutoa elimu ya kujikinga na corona wakati wote...na pia wataalamu wa afya nendeni katika redio zote zilizopo mkoani Tabora kupeleka ujumbe ambao utawasaidia wananchi kuepuka kupata maambukizi ya corona,” alisema Mwanri.

CHAMA cha ADA- Tadea kimesema kitendo cha Mbunge wa Kawe, ...

foto
Mwandishi: Tiganya Vincent, Tabora

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi