loader
Picha

Simbachawene kuifumua Nida

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema watafanya mabadiliko makubwa kwenye Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) kwa kuwaondoa watumishi wasio na nidhamu kwenye kazi.

Kwa mujibu wa waziri huyo, mpaka sasa Watanzania milioni sita tu ndio waliopata vitambulisho vya taifa kati ya Watanzania milioni 27 wanaostahili kupata vitambulisho hivyo.

“Tutafanya mabadiliko makubwa ndani ya Nida, mamlaka ya ajira itateua Watanzania wengine wenye sifa za kufanya kazi hiyo. Zimeripotiwa taarifa za baadhi ya watendaji ambao hawatoi huduma kama inavyostahili kwa wananchi, niwahakikishie hili hatutalifumbia macho watachukuliwa hatua kali kwa kila atakayebainika,” alisema.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana jijini hapa, Simbachawene alisema Nida sasa inaendelea na zoezi la usajili, utambuzi na ugawaji wa vitambulisho vya taifa kwa Watanzania, pamoja na wageni wakazi na wakimbizi waishio nchini kihalali.

Alisema katika hilo, Nida inashirikiana na Idara ya Uhamiaji, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) na Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (ZCSR) lakini kwenye baadhi ya maeneo hasa wilayani watumishi wa Nida wamekuwa wakifanya kazi kivyaovyao bila kushirikisha mamlaka mengine.

“Nikiri tu kwamba ipo changamoto ndani ya Nida na inahitaji kushughulikiwa na tutafanya mabadiliko makubwa kuanzia sasa. Nichukue nafasi hii kukiri mbele ya watanzania zoezi letu limesuasua lakini mpaka mwisho wa mwezi wanne tutakuwa tumekamilisha kufunga mtambo mpya ambo utakuwa na uwezo wa kutoa vitambulisho 9,000 kwa saa moja,” alisema Simbachawene.

Alisema kumekuwa na changamoto nyingi wakati wa uendeshaji wa zoezi hilo ikiwemo wananchi kuambiwa sio raia na kuzua sintofahamu kwa wananchi hao ambapo pia watumishi hao wamekuwa wakiwajibu wananchi wanavyotaka jambo ambalo halikubaliki. Pia alisema kuna changamoto mbalimbali zilizojitokeza ikiwemo watumishi hao kwenye baadhi ya maeneo wakifika hutaka kufanya kazi paipo kushirikiana na mamlaka husika ikiwemo mamlaka za vijiji na mitaa.

Alisema mpaka sasa watu 21,823,026 wamejitokeza na kusajiliwa, kufikia Machi 27 mwaka huu, kati ya watu 27,796,983 waliotarajiwa kusajiliwa. Pia moja ya matumizi ya utambuzi ni katika usajili wa laini za simu ambapo hadi Machi 27, mwaka huu, jumla ya namba za kipekee za utambulisho wa taifa ni 17,860,284 zilikuwa zimezalishwa na zinaweza kutumika katika utambuzi wa watu.

Alisema pamoja na changamoto zilizojitokeza, wizara inaendelea kuweka msisitizo kwa nguvu zote kuhakikisha zoezi hilo linaenda vizuri na kwa kasi.

CHAMA cha ADA- Tadea kimesema kitendo cha Mbunge wa Kawe, ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi