loader
Picha

Polisi wanaoshirikiana na wauza ‘unga’ waonywa

JESHI la Polisi limesema limejipanga kuhakikisha biashara ya dawa za kulevya inatokomezwa nchini na kuwaonya askari wake watakaobainika kushirikiana na wanaojihusisha na vitendo hivyo kuwa onyo hilo lilitolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspeka Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro, wakati akifungua kituo cha Polisi Nungwi, mkoa wa Kaskazini Unguja juzi.

Alisema biashara ya dawa za kulevya haikubaliki nchini na kwamba Jeshi la Polisi limejipanga kuitokomeza na wahusika wake kukamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

‘’Jeshi la Polisi tumejipanga kuhakikisha kwamba biashara ya dawa za kulevya haina nafasi tena nchini, lakini pia tunawataka askari wetu wasijishughulishe na biashara hiyo na watakaobainika wajue kwamba watafukuzwa kazi,’’ alisema.

Aidha, Sirro aliwataka watalii katika ukanda wa Kaskazini Unguja wasijishughulishe na biashara ya dawa za kulevya kwani watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria. Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Vuai Mwinyi, alilipongeza Jeshi la Polisi kwa kuweka kituo cha polisi katika jimbo la Nungwi lenye idadi kubwa ya hoteli za kitalii. Alisema kuwapo kwa kituo hicho, kutasaidia kudhibiti na kupunguza matukio ya uhalifu kwa watalii pamoja na hoteli zake.

‘’Serikali ya mkoa wa Kaskazini Unguja tumefurahishwa sana na ujenzi wa kituo hiki ambacho matarajio yetu makubwa kitasaidia kupunguza uhalifu katika sekta ya utalii,’’ Naye, Kamishna wa Jeshi la Polisi Ushirikishwaji Jamii, Mussa Ali Mussa, aliwataka wananchi kukitumia kituo hicho kwa ajili ya kutoa taarifa mbalimbali za matukio ya kihalifu.

‘’Lengo la ujenzi wa kituo hiki ni kuzipatia ufumbuzi changamoto za wananchi zinazohusu matukio ya uhalifu wa aina mbalimbali na kupatiwa ufumbuzi wa kudumu,” alisema.

Ujenzi wa kituo cha polisi katika kijiji cha utalii cha Nungwi umegharimu Sh milioni 64 na unatokana na kilio cha muda mrefu cha wananchi na wawekezaji kutaka kuwapo kwa kituo hicho kitakachosaidia kupambana na matukio ya uhalifu ikiwamo wizi katika hoteli za kitalii.

WABUNGE wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),akiwemo Wilfred ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi