loader
Picha

Pemba yatenga maeneo 4 wagonjwa corona

MAENEO manne yametengwa kwenye kisiwa cha Pemba kwa ajili ya tahadhari ya kuwaweka wagonjwa watakaobainika kuugua homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona.

Ofisa Mdhamini wa Wizara ya Afya Pemba, Shadya Shaaban Seif, ameyataja maeneo hayo kuwa ni Mfikiwa eneo la kambi ya Red Cross wilaya ya Wete Pemba, Hospitali ya Abdalla Mzee, Ungi Msuka na Micheweni, mkoa wa Kaskazini Unguja.

‘’Kwa upande wa kisiwa cha Pemba tayari tumetenga maeneo manne ya kuwahifadhi wagonjwa watakaobainika kuugua homa hiyo,’’ amesema.

Amesema maandalizi yote ya vituo hivyo kwa ajili ya kupokea wagonjwa hao yamekamilika na kuwataka wananchi kuondoa hofu. Shadya aliwataka wananchi watakaojihisi kuwa na dalili za virusi vya corona haraka kufika katika vituo vya afya na kuchunguzwa afya zao.

Aidha, aliwataka wananchi kuchukua tahadhari kwa wageni wanaoingia nchini, kwamba wanafuata masharti ikiwamo kupima afya zao na kujitenga na familia kwa muda wa siku 14.

‘’Hayo ndiyo masharti ya afya yanayotolewa na Wizara ya Afya, ambapo wananchi wanatakiwa kuyafuata na kuyazingatia kwa kina ili kujikinga na virusi vya corona na Naibu Waziri wa Afya, Harusi Suleiman Said, ambaye ametembelea vituo hivyo alisema ameridhishwa na maandalizi yake na sasa vipo tayari kupokea wagonjwa watakaobainika kuambukizwa virusi vya corona.

Alitaka tahadhari zaidi zichukuliwe ikiwamo maeneo ya bandarini ili kudhibiti wageni wanaoingia katika kisiwa hicho bila ya kuchunguzwa afya zao.

‘’Tunawaomba wakuu wa mikoa na kamati za ulinzi kudhibiti uingiaji wa watu kupitia bandari mbalimbali kwa sababu tunafahamu wananchi wa kisiwa cha Pemba wanayo mahusiano na watu wengi wanaoishi Tanzania Bara na Mombasa, Kenya,’’ amesema.

MTANDAO wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia (MKUKI) umesema wasichana 40 ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

1 Comments

  • avatar
    mohammed
    03/04/2020

    Mimi ni muunguja. Naomba kwa mwenyezi mungu atuweke salaama na atupe afya njema.

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi