loader
Picha

Mwanri aagiza walimu wa tuisheni wasakwe

MKUU wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, ameagiza kusakwa kwa walimu ambao wamekuwa wakiwakusanya wanafunzi kwa ajili ya kufundisha masomo ya ziada kwa kuwa wanapingana na kampeni ya kudhibiti na kupambana na ugonjwa wa corona (Covid -19).

Hatua hiyo inalenga kuzuia mazingira yanayoweza kusababisha wanafunzi hao kupata virusi vya corona. Mwanri alitoa agizo hilo jana wilayani Nzega, wakati wa ziara yake ya kukagua vituo na zahanati zilizoandaliwa kwa ajili ya washukiwa wa ugonjwa wa corona mkoani humo.

“Ni marufuku kwa walimu kutumia janga la ugonjwa wa corona kujipatia maslahi, kwani kufanya hivyo ni kuvunja sheria kwa kisingizio kuwa wanawafundisha watoto masomo ya ziada.”

“Baadhi ya wamiliki wa shule binafsi ndio wanasababisha walimu kujiingiza kwenye ufundishaji wa tuisheni baada ya kuwaambia kuwa hawatawalipa mshahara kwa sababu hawafundishi katika kipindi hiki ambacho shule zimefungwa kutokana na covid -19.”

“Hilo halikubaliki na ndio linalowafanya baadhi yao kujiingiza katika ufundishaji wa tuisheni kinyume cha maagizo ya serikali katika kukabiliana na covid-19,” alisema.

Mwanri alisema ni lazima walimu wote walipwe mishahara yao ili kutowaweka katika vishawishi vya kujiingiza katika kuvunja maagizo ya serikali ya kuzuia mikusanyiko kwa wanafunzi.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk Honaratha Rutatinisibwa, amewataka wazazi kutowaruhusu watoto wao kuzurura ovyo mitaani kwani kunaweza kuwasababisha kupata maambukizi ya virusi vya corona.

WABUNGE wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),akiwemo Wilfred ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Tabora

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi