loader
Picha

Jafo- Naanza kuiona Hospitali ya Uhuru

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo ameonesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi unaoendelea katika Hospitali ya Uhuru inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Mkoani Dodoma.

Akizungumza baada ya kutembelea eneo la ujenzi, Jafo alisema: “Angalau sasa naanza kuiona Hospitali ya Uhuru, naamini baada ya wiki mbili kuja kitu kitaonekana hapa.

“Nimeridhika na kasi ya ujenzi unaoendelea katika Hospitali ya Uhuru na hasa nimefurahishwa na utekelezwaji wa maagizo yangu niliyoyatoa ya kuongeza nguvu kazi, sasa naona kuna nguvu kazi ya watu 300 ambao ni tofauti na awali walikuwa 100,” amesema.

Jafo aliuagiza uongozi wa Suma JKT kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa hospitali hiyo ili kuweza kukamilisha kazi hiyo kwa wakati uliopangwa.

Pia aliutaka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kuwa na mpango kazi wa manunuzi ya vifaa ili kuhakikisha vifaa vya ujenzi vinakuwa sioa sababu ya kukwamisha ujenzi wa hospitali hiyo.

Mhandisi wa SUMA JKT, Omary Kabalangu alisema kuwa tayari wametekeleza maagizo yake ya kuongeza nguvu kazi kutoka watu 100 wa awali hadi kufikia 300, sambamba na kuongeza muda wa kufanya kazi kwa kujenga usiku na mchana,

“Kwa kutekeleza maagizo uliyotupa, kumefanya kupunguza wiki tatu kati ya wiki tisa ambazo tulikuwa tuko nyumba ya muda wa mkataba, na imani yetu muda uliopotea tutaendelea kuupunguza.” amesema.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Athumani Masasi alisema ofisi yake imejipanga kuhakikisha saruji na nondo na vifaa vingine vya kutosha vinakuwa eneo na ujenzi na hilo linakuwa siko kikwazo.

Pia amemshukuru Rais John Magufuli kwa maono yake ya kujenga hospitali hiyo kubwa kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa watanzania na wananchi wa nchi za jirani.

Hospitali ya Uhuru inajengwa kwa gharama ya Sh bilioni 3.99, fedha zilizotolewa na Rais Magufuli baada ya kuahirisha Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Uhuru Desemba 9 mwaka 2018 na zile zilizotokana na gawio la kampuni ya Airtel.

WABUNGE wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),akiwemo Wilfred ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi