loader
Picha

Walimu msingi, sekondari wapanda daraja

WALIMU 151 wa shule za msingi na sekondari Manispaa ya Lindi wamepandishwa madaraja na kupewa mishahara mipya tangu mwaka 2016.

Katibu wa Chama cha Walimu (CWT) Lindi, Nassoro Mwinshehe amesema hayo jana wakati akizungumza na HabariLEO mjini hapa.

Alisema walimu hao walipandishwa madaraja baada ya uhakiki uliofanyika kati ya mwaka 2016 na kurekebishiwa kwa mishahara yao.

‘’Kwangu hakuna tatizo la upandaji wa madaraja wakati huu, walishafanyiwa marekebisho ya mishahara mipya kulingana na daraja,’’ amesema.

Amesema kuna madeni tangu mwaka 2018 hadi mwaka huu ya Sh 128,132,164 hayajalipwa.

Alisema walimu wanadai fedha za uhamisho Sh 85,496,000, mapunjo ya mishahara Sh 6,664,000, matibabu Sh 7,174,000.

Alisema madai ya walimu masomoni ni Sh 9,920,000, kujikimu Sh 954,000, wastaafu wanadai Sh 6,664,000, mengine Sh 26,720,000.

Alisema uteuzi wa walimu wakuu shule za sekondari na msingi unafanywa kirafiki hali inayosababisha kuwepo kwa migongano ya walimu na walimu wenzao katika shule moja.

WABUNGE wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),akiwemo Wilfred ...

foto
Mwandishi: Kennedy Kisula, Lindi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi