loader
Picha

'Msiwaonee aibu wenye mzaha janga la corona'

VIONGOZI wa dini katika mkoa wa Tabora wameiomba serikali kutowaonea aibu wale wote wanaoleta mzaha na kutafuta umaarufu kupitia janga la ugonjwa wa homa ya mapafu, corona.

Kauli hiyo ilitolewa jana wakati wa maombi na dua maalumu ya viongozi wa dini na Serikali ya Mkoa wa Tabora kuuweka Mkoa wa Tabora, taifa na dunia nzima mikononi mwa Mungu ili awakinge na janga la ugonjwa wa Covid-19.

Mchungaji wa Kanisa la Agape Miracle Centre, Elias Mbagata amesema bado kuna mizaha juu ya janga hilo.

Ameiomba serikali isiwaonee haya watu hao hata kama ni viongozi wakubwa.

Alisema kinachotakiwa kufanywa sasa ni kuwajengea matumaini wananchi badala ya kuwajaza hofu na kufanya wachanganyikiwe.

Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tabora, Dk Elias Chakupewa alisema walichukua hatua kuwaelimisha waumini wao kufuata taratibu zinazotakiwa ikiwemo maelekezo ya wataalamu na viongozi wa serikali namna sahihi ya kujikinga na Corona.

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Tabora, Askofu Paul Ruzoka amewaomba waumini kuungana na serikali kupigana vita hii kwa kuhakikisha wanatekeleza maelekezo yanayotolewa na viongozi na wataalamu wa afya.

Amesema kanisa hilo limesitisha kwa muda baadhi ya taratibu za kuendesha ibada, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuungana na Serikali katika mapambano dhidi ya Covid -19.

WABUNGE wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),akiwemo Wilfred ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Tabora

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi