loader
Picha

Waweka uzio kwenye mabwawa kuokoa watoto

BAADHI ya wananchi wa Kijiji cha Kangeme, Ulowa na Namba nne katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameanza kufukia mashimo na kuweka uzio mabwawa ya kunyweshea mifugo ili kuepusha vifo vya watoto.

Imedaiwa watoto wawili, mmoja wa miaka mitano na mwingine miwili walitumbukia kwenye madimbi yaliyokuwa yamejaa maji Machi mwaka huu katika kijiji cha namba nne.

Mwenyekiti wa kijiji cha Namba nne, Paul Shinji ameyasema hayo kijijini hapo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi.

Amesema ufukiaji madimbwi ulianza Machi mwaka huu na kuwataka wanaomiliki mabwawa ya kunyweshea mifugo waweke uzio kuepuka vifo vya watoto vitokanavyo na kutumbukia.

“Kamati ya ulinzi na usalama ya kijiji tulipita Machi mwishoni kukagua kama wametekeleza ufukiaji madimbwi na kujenga uzio kwenye mabwawa, wameanza kutekeleza,” alisema.

Mwenyekiti Shinji alisema mashimo hayo waliyokuwa wameyachimba kwa umwagiliaji wa mbegu za tumbaku kiangazi yafukiwe kwani watoto walitumbukia wengine kupona na baadhi kupoteza maisha kipindi hiki cha mvua.

Diwani wa Kata ya Ulowa, Paschal Mayengo alisema ulinzi na usalama kwa watoto na elimu kwa wazazi katika mikutano ya hadhara na mashirika yasiyo ya kiserikali vimesaidia.

Alisema matukio ya watoto chini ya umri wa miaka mitano kufariki dunia katika madimbwi ndiyo yalikuwa yanaleta majonzi kila mara.

“Sasa tumefukia madimbwi na mabwawa ya kunyweshea mifugo yawekewe uzio na wamiliki wameanza kutekeleza sababu utakuta nyuma ya nyumba ya mtu kuna dimbwi na watoto wanacheza pembeni jambo ambalo ni hatari. Kuwalinda tunayafukia yote,” alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha alisema lazima mzazi awajibike kwa ulinzi na usalama wa mtoto wake ipasavyo.

Alitaka wazazi washirikiane na jamii na kama kuna viashiria vya kuhatarisha maisha ya watoto maeneo ya kuchezea pawepo mikakati kudhibiti.

WABUNGE wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),akiwemo Wilfred ...

foto
Mwandishi: Kareny Masasy, Ushetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi