loader
Picha

Mil 23/- zanunua pikipiki za watendaji, manispaa

HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imenunua pikipiki saba zenye thamani ya Sh milioni 23.1 kwa fedha za Mradi wa Uboreshaji Miji (ULGSP) bajeti ya mwaka wa fedha 2019/ 2020 kuwezesha watumishi kuboresha utendaji.

Meya wa Manispaa ya Morogoro, Pascal Kihanga aliwaambia hayo waandishi wa habari baada ya pikipiki aina ya Yamaha kukabidhiwa.

Kihanga alisema pikipiki nne zimetolewa kwa watendaji katika kata nne zilizo pembezoni za Luhungo, Mzinga, Mkundi na Kingolwira.

Alisema pikipiki tatu zilitolewa kwa ajili ya Ofisi Kuu ya Manispaa ili kutumiwa katika kuimarisha utendaji kazi wa halmashauri.

“Tumenunua pikipiki hizi kwa ajili ya kata hizi za pembezoni zenye changamoto, watendaji wake wanashindwa kuwafikia wananchi kwa urahisi na kushindwa kutoa huduma,” alisema.

Mkurugenzi wa Manispaa, Sheilla Lukuba alisema imenunua pikipiki hizo kurahisisha huduma bora kwa wananchi katika kata hizo.

Amesema ni matarajio ya halmashauri kuona pikipiki hizo zinarahisisha kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa shughuli za serikali kwani hata maeneo yasiyofikika kwa urahisi gari yatafikika.

“Tuvitunze vyombo hivi, tuvipe heshima na kuvitumia kwa malengo. Tusiende kuvigeuza bodaboda. Tutaweka utaratibu na atakayekiuka tutamchukulia hatua kali za kisheria,” amesema.

Watendaji wa kata zilizopatiwa pikipiki hizo waliushukuru uongozi wa Manispaa kutambua changamoto zinazowakabili na kuongeza bidiii kuwahudumia wananchi kuwaletea maendeleo.

WABUNGE wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),akiwemo Wilfred ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi