loader
Picha

Mfanyabiashara adaiwa kujitosa Mto Rufiji

 

Mmoja wa wanafamilia hao ambaye hakutaka kuandikwa jina gazetini amesema, ndugu yake alipiga simu na kusema hawatamuona tena na kwamba waende Mto Rufiji katika daraja la Mkapa watakuta taarifa zake.

Amesema, baada ya kufika eneo hilo, walikuta kofia yake, simu mbili na barua ambayo ndani yake ilikuwa na maelezo ya wosia yanayodhaniwa kuandikwa na ndugu yao huyo.

Alisema katika barua hiyo, mfanyabiashara huyo alielekeza mgawanyo wa mali zake ambazo ni duka alilotaka wapewe wanawe, huku akitaka kuuzwa kwa shamba moja ili kuendeleza mengine yaliyopo.

Alisema bahasha ya barua hiyo ilikutwa pembezoni mwa mto huo na kwamba wanahisi amejitosa ndani ya mto huo kutokana na sababu ambazo hata hivyo hakuzieleza katika wosia huo.

Alisema baada ya kukuta barua na vitu hivyo waliamua kwenda kutoa taarifa hizo polisi, ambao walienda eneo la tukio na na barua hiyo.

Kamanda Lyanga alisema Jeshi la Polisi limepokea taarifa za kupotea kwa mfanyabiashara huyo, lakini hakuwa tayari kuthibitisha kifo chake kutokana na kukosa uhakika wa kifo hicho.

WABUNGE wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),akiwemo Wilfred ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Rufiji

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi