loader
Picha

Wabunge wataka elimu zaidi ya corona

HOJA ya mapambano dhidi ya homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (Covid-19) pamoja na udhibiti wake, imetawala katika mjadala wa bajeti ya Ofi si ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2020/21.

Wakichangia bungeni jana bajeti hiyo, wabunge waliitaka serikali iweke mkazo zaidi na kueleza jitihada zaidi za kupambana na virusi hivyo, ili kuepuka athari kubwa, kama zilizojitokeza kwenye mataifa makubwa. Mbunge wa Moshi Mjini, Jafari Michael (Chadema), alishauri jitihada za kudhibiti corona ziendelee, ikiwemo kupata fedha kupitia njia yoyote ya kibajeti na ambazo sio za kibajeti za kutumia wadau.

“Fedha hizi zinunue vipimo vya upimaji ili tujue kwa kiwango gani watu wameathirika kwa janga hili, mpaka sasa tunaamini tuna watu wachache sana ambao ni wagonjwa hatuna uhakika kwa avipimo, inaonekana kuna wagonjwa bado wapo ndani, ni vyema tukapima ili kujua k iwango cha maambukizi na kukabiliana nacho kabla ya kuruhusu kuwa kubwa kwa jamii yetu,” alisema Michael.

Michael alishauri serikali kuangalia athari za virusi hivyo kiuchumi huku akisema sekta ya utalii imeathirika zaidi. Mbunge wa Njombe Mjini, Edward Mwalongo aliitaka serikali kuwaandaa Watanzania na kuwaelimisha yanayoendelea duniani kuhusu virusi hivyo; na watambue kama hali itakuwa mbaya, wajue bayana watatakiwa kukaa ndani.

Kwa upande wake, Mbunge wa Iramba Mashariki, Allan Kiula (CCM) alishauri bajeti ya ofisi hiyo na wizara nyingine, zitumie fedha zitakazopatikana kwenye maeneo muhimu, kwani Covid-19 inaweza kusababisha upatikanaji wa fedha usiwe mzuri.

“Kwa kuwa hatuna hakika kama ‘flow” (mtiririko) itakuwa nzuri kama tunavyoona nchi zingine, ni vyema fedha zitakazopatikana zielekezwe kwenye mambo muhimu, pia kwenye suala la kukaa kwa umbali bado linatupa shida kidogo,” alisema Kiula. Mbunge wa Korogwe Mjini, Mary Chatanda (CCM) alisema bado kuna maeneo wananchi wanahitaji kupewa elimu zaidi.

Alitaja maeneo hayo kuwa ni stendi, masoko na mabaa. Pia alisema elimu zaidi, inapaswa kutolewa kuhusu suala la misongamano.

“Bado tunaona kwenye stendi, masoko kuna misongamano, watu bado wanakutana na kukaa kwenye mabaa na sehemu za starehe, kwa hiyo bado bado elimu na mkazo zaidi unatakiwa,” alisema Chatanda.

Hoja hiyo iliungwa mkono na Mbunge wa Viti Maalumu, Cecilia Pareso (Chadema) ambaye alisema juhudi zaidi zinahitajika, kukabiliana na misongamano hasa katika maeneo ya stendi, masoko, magereza na mahabusi za Polisi, ambako mkusanyiko wa watu ni mkubwa.

Pareso alisema kama Covid- 19 itazidi, hali ya uchumi itatereka hivyo serikali ilete taarifa au ripoti ya athari ya kiuchumi, itakayotokana na athari za virusi vya corona. Mbunge wa Mtambile, Masoud Abdalah Salim (CUF), aliwaasa Watanzania kuacha dhambi, kwa kuwa dunia imesimama kwa sababu ya corona.

“Ni vyema mkakati ukaongezwa zaidi kukabiliana na corona, vitakasa mikono bei zake zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku, jambo hili ni kubwa, hakuna vitakasa mikono, elimu na barakoa vijijini, serikali iangalie jambo hili,” alisema Salim.

Aliiomba serikali iongeze vipimo zaidi vya kuwatambua washukiwa wa ugonjwa huo, badala ya kutumia maabara iliyopo Hospitali ya Muhimbili. Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema) alisema kwa kuwa suala la corona, lipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, watu wanapaswa kufahamu kuwa si suala la kiimani ni la kisayansi.

“Corona inaua na itaua mamilioni hatua zisipochukuliwa hivyo watu wasilete siasa kwenye hili…tuungane kukabiliana nalo, sio tatizo la Ummy na Wizara ya Afya, bali mawaziri wote wanahusika sababu biashara zinakufa,” alisema Mbilinyi.

Aliongeza kuwa njia bora ya kuidhibiti corona ni kudhibiti isisambae. Aliwataka viongozi kumwaga dawa barabarani ili isisambae sana, maana ikitokea hivyo, majanga yatakuwa makubwa.

Mbunge wa Kalenga, Godfrey Mgimwa (CCM), alisema ugonjwa wa Covid- 19 umesababisha athari za kiuchumi kwenye mataifa yenye uchumi mkubwa na wameshindwa kuuzuia. “Je, serikali imejipangaje kukabiliana na ugonjwa huu, ukipita maeneo ya starehe vijana wapo kuanzia saa moja hadi saa nane usiku, tukishindwa kuzuia maeneo hayo sijui tutakuwa na hali gani?,”alihoji.

WABUNGE wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),akiwemo Wilfred ...

foto
Mwandishi: Angela Semaya, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi