loader
Picha

Kubenea: Sina mpango wa kuondoka Chadema

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema) amesema hana mpango wa kuondoka kwenye chama chake. Ameshutumu wanaomtabiria kuwa atamfuata Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu aliyetangaza kukihama chama hicho atakapomaliza ubunge.

Aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kwamba Komu ni rafiki na nduguye, lakini hiyo haimaanishi kila analofanya, naye lazima alifanye.

“Ramli ziachwe, mimi mpaka sasa ni Mbunge wa Chadema, nahitaji kutumikia wananchi hadi mwisho,” alisema Kubenea katika mkutano huo, ambao pia aliwataka wananchi kuchukua hadhari dhidi ya corona.

Kubenea alisema sasa anawatumikia wananchi, waliomchagua na muda ukifika na zaidi baada ya corona kuisha, ndipo atakuwa katika nafasi ya kuzungumzia masuala ya ubunge.

Akijibu maswali ya waandishi juu ya mwenendo wake katika chama, ikiwamo kutokukubalika miongoni mwa wanachama, alisema Chadema ni taasisi kubwa, hivyo si ajabu kuwepo ushindani wa kimya kimya ndani ya chama hata jimboni kwake.

Kubenea ametoa msimamo wake ndani ya chama siku chache baada ya Komu kutangaza kwamba ataihama Chadema, baada ya kipindi chake cha ubunge kumalizika na atahamia NCCR-Mageuzi. Akizungumzia mikakati ya kukabili maambukizi ya corona, Kubenea alipongeza juhudi zinazofanywa na serikali.

Alisisitiza kuwa wananchi wawe na mshikamano bila kujali itikadi za vyama na dini. Alishauri mikusanyiko yote, ikiwamo ibada na mazishi izuiwe na hali ikiendelea kuwa mbaya pia Bunge lisitishe vikao vyake.

CHAMA cha ADA- Tadea kimesema kitendo cha Mbunge wa Kawe, ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi