loader
Picha

Miradi ya maji miji 26 ikamilishwe - wabunge

WABUNGE wameiomba serikali ikamilishe miradi midogo ya maji katika miji 26, iliyoahidiwa kupewa maji kupitia mradi mkubwa, uliokuwa utekelezwe kwa fedha kutoka India.

Walisema hayo bungeni jijini hapa jana wakati wakichangia hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2020/2021.

Mbunge wa Njombe Mjini, Edward Mwalongo alisema miji hiyo ilipewa ahadi ya kupewa maji kupitia fedha za mradi kutoka India, lakini ni miaka miaka mitano sasa miji hiyo haijapata maji.

“Tatizo la maji ni kubwa, tuliahidiwa miji 26 kupata maji kupitia fedha za mradi kutoka India, lakini miaka mitano sasa hakuna kitu, imekuwa hadithi tu…lini sasa miji hii itapata maji?” alihoji Mwalongo.

Akichangia zaidi, aliiomba serikali ibadilishe utaratibu kama nchi, wizara husika itafute namna ya kuipatia miji hiyo maji wakati fedha hizo kutoka India zikisubiriwa. Mbunge wa Korogwe Mjini, Mary Chatanda (CCM) akichangia hoja hiyo ya maji, alisema Wizara ya Maji ilitoa miradi midogo, lakini mengine haijakamilika na kuitaka iikamilishe wakati ikisubiriwa miradi mikubwa.

“Naomba miradi hii midogo ikamilishwe ili wananchi wapate maji kabla ya mradi huo wa India ambao umesemwa muda mrefu lakini haufiki,” alisema Chatanda.

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Kiembesamaki, Ibrahim Raza (CCM) ameiomba serikali kipindi hiki kuna tishio la virusi ya corona, iangalie uwezekano wa kusitisha kodi ya maji kwa miezi mitatu kuanzia ngazi ya chini hadi juu, kwa sababu maji yanatumika kwa wingi. Raza alisema Watanzania wengi wanahitaji maji hasa muda huu, hivyo ni vema yapatikane kwa wingi na kwa urahisi.

CHAMA cha ADA- Tadea kimesema kitendo cha Mbunge wa Kawe, ...

foto
Mwandishi: Angela Semaya, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi