loader
Picha

Serikali yaandaa rasimu kulinda vyanzo vya maji

SERIKALI kupitia Ofi si ya Makamu wa Rais imeandaa rasimu ya mwongozo wa mita 60 wa kuhifadhi vyanzo vya maji.

Hayo yalielezwa kwenye majibu ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kutokana na swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Zainabu Amiri (CUF). Rasimu hiyo inaainisha matumizi endelevu ya eneo la mita 60 kutoka vyanzo vya maji ikiwemo shughuli za kilimo kando na vyanzo vya maji Hata hivyo, kifungu cha 57 cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004 kinazuia shughuli za kudumu na ambazo kwa asili yake inaweza kuhatarisha au kuathiri vibaya utunzaji wa bahari au kingo za mto, na mabwawa katika eneo la hifadhi mita 60 kutoka vyanzo vya maji.

Aidha, sheria hii inampa mamlaka waziri mwenye dhamana ya usimamizi wa mazingira kuandaa mwongozo wa matumizi endelevu wa eneo hilo. Katika swali lake la msingi, Amiri alisema: “Mboga za majani ni lishe bora kwa afya ya binadamu; na wakulima wengi wa mboga hasa jijini Dar es Salaam wanatumia maji yasiyo salama kwa ajili ya kumwagilia na huenda maji hayo yana kemikali zinazoweza kupelekea mbogamboga hizo kudhuru afya za wananchi badala ya kuziimarisha.

Hivyo, Amiri alitaka kujua mpango wa serikali wa kuwapatia maji safi na salama wakulima hao wa mboga. Majibu ya swali hilo, Ofisi ya Makamu wa Rais imekiri kuwa wakulima wengi wa mboga za majani waliopo Jiji la Dar es Salaam hutegemea Bonde la Mto Msimbazi kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao.

“Hata hivyo, mto Msimbazi unaendelea kukabiliana na changamoto za uharibifu wa mazingira unaosababishwa na shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwemo kilimo cha mboga kando ya mto huo,” ilieleza.

Aidha, serikali kwa kushirikiana na wadau imeendelea kutoa elimu kuhusu hifadhi ya vyanzo vya maji na kutekeleza mipango na shughuli mbalimbali kwa ajili ya kulinda mazingira ya mto huo yasiharibiwe.

Majibu ya Ofisi ya Makamu wa Rais yamebainisha kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeandaa mradi wa kuboresha Bonde la Mto Msimbazi ili kukabiliana na changamoto zitokanazo na uharibifu wa mazingira katika mto huo.

MTANDAO wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia (MKUKI) umesema wasichana 40 ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi