loader
Picha

TCRA kukagua ubora wa huduma za mawasiliano

SERIKALI kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) itafanya ukaguzi wa ubora wa huduma za mawasiliano kulingana na viwango vya ubora ili kuhakikisha wananchi wanapata mawasiliano ya uhakika.

Hayo yameelezwa kwenye majibu yalitotolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakati wa kujibu swali la msingi la Mbunge wa Sikonge, Joseph Kakunda (CCM).

“TCRA kwa kushirikiana na watoa huduma inafanya ukaguzi kulingana na viwango vya ubora vilivyowekwa kwa mujibu wa Kanuni za Ubora ili kuhakikisha wananchi wanapata mawasiliano ya uhakika kwa maeneo yenye usikivu hafifu,” ilieleza taarifa ya wizara hiyo.

Katika swali lake la msingi, Kakunda alitaka kujua ni lini serikali itawapatia mawasiliano ya uhakika wakazi wa Sikonge wanaoishi kwenye kata zenye minara ya simu lakini isiyokamata mtando vizuri.

Pia alitaka kujua serikali itawapatia lini mawasiliano ya simu wananchi wa Sikonge ambao wanaishi kwenye kata ambazo hazina kabisa minara ya mawasiliano ya simu.

Katika majibu ya swali hilo, wizara imeelezea kuwa serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote imetoa ruzuku kwa ajili ya ujenzi wa minara ya mawasiliano katika Wilaya ya Sikonge katika kata za Kiloli, Igigwa, Kipanga, Kipili na Kitunda.

WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imeweka mkakati wa upatikanaji wa ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi