loader
Picha

Wasafiri 84 kutoka Afrika Kusini wawekwa karantini

KATIKA kutekeleza maagizo ya serikali ya kuhakikisha wasafi ri wote wanaotoka katika nchi zenye maambukizi zaidi ya virusi vya corona wanatengwa, jumla ya wasafi ri 84 kutoka Afrika Kusini wamewekwa karantini kwa muda wa siku 14 katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Nicodemus Mwangela aliyasema hayo alipofanya ukaguzi wa maandalizi ya utayari wa kupambana na homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (Covid-19) kwa Mkoa wa Songwe hususani maeneo ya mipakani katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje na Halmashauri ya Mji wa Tunduma.

Mwangela alisema wasafiri hao ambao ni Watanzania 55 na raia wengine kutoka Congo, Afrika Kusini, Kenya na Uganda walipoingia nchini kupitia mpaka wa Tunduma walipimwa na kukutwa hawana dalili za virusi vya corona na kwa kuwa wametoka katika nchi yenye maambukizi zaidi wametengwa katika karantini.

Aliagiza Jeshi la Polisi kufanya msako katika maeneno ya stendi za mabasi endapo kutakuwa na raia kutoka katika nchi zenye maambukizi zaidi ya virusi vya corona na wamepitia njia zisizo rasmi wawekwe karantini.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa, George Kyando alisema jeshi hilo limepiga marufuku kwa mabasi kujaza abiria kuliko uwezo wa gari, kutokuwa na vitakasa mikono kwenye mabasi au maji na sabuni kwa ajili ya kunawa na marufuku ya mabasi kuanza safari bila kupuliziwa dawa.

Alisema yeyote atakayepuuzia marufuku hizo zilizolenga kuweka tahadhari ya kutosambaza corona atakuwa anataka kusambaza kwa makusudi jambo ambalo ni kosa kisheria hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma, Dk Enock Mwambalaswa alisema wasafiri wote waliowekwa karantini wanapimwa mara mbili kwa siku ili kufuatilia maendeleo ya afya zao na endapo atatokea mwenye dalili za corona hatua za haraka zitachukuliwa lakini hadi sasa wote wanaendelea vizuri na hakuna aliyebainika.

CHAMA cha ADA- Tadea kimesema kitendo cha Mbunge wa Kawe, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Ileje

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi