loader
Picha

Latra yaruhusu watu binafsi kusafirisha abiria

ZIKIWA ni siku chache tangu serikali kupiga marufuku usimamishaji wa abiria katika daladala na mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, Mamlaka ya Udhibiri wa Usafi ri Ardhini (Latra), imetoa wito kwa watu binafsi, shule na taasisi zenye mabasi ambayo hayajapangiwa njia kuomba leseni za muda mfupi kutoa huduma za usafi ri.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Latra jana, Gilliard Ngewe, watu wenye mabasi ya abiria ambao hawaja- pangiwa njia ku- fika ofisi za Latra kuomba leseni za kuanza kutoa huduma hiyo.

Hivi karibuni, Latra iliagiza mabasi yote yaendayo haraka (BRT) na daladala zote kubeba abiria kulingana na idadi ya viti vilivyopo ukiwa ni mkakati wa kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.

Pia iliagiza kila chombo cha usafiri iwe na dawa ya kuua virusi mikononi kabla ya abiria kuingia ndani ya basi asafishe mikono kwa dawa ya kuua virusi mikononi.

Ngewe alisema utekelezaji wa agizo ni hatua ya kujikinga dhidi ya virusi vya Corona katika vyombo vya usafiri. Aliwataka pia Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara) kuhakikishq treni zinapulizwa dawa kila mwisho wa safari.

Mbali na hilo kwa magari ya mizigo, Ngewe alisema hayaruhusiwi kubeba abiria yeyote huku akisistiza elimu juu ya kujikinga na Corona itolewe ndani ya vyombo vya usafiri kwa kutumia redio na runinga katika magari hayo.

CHAMA cha ADA- Tadea kimesema kitendo cha Mbunge wa Kawe, ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

1 Comments

  • avatar
    Mzee magimba
    03/04/2020

    Hilo ni wazo zuri sana kwani litasaidia sana kuondoa misururu kwenye vituo vya mabasi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi